Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wanaCCM na wananchi mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa tanki la maji katika kata ya Isengwa wilayani Meatu mkoa wa Simiyu leo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa tanki la maji katika kata ya Isengwa wilayani Meatu mkoa wa Simiyu leo.
(PICHA JOHN BUKUKU NA ADAM MZEE WA CCM)
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa RUWASA Meatu Mhandisi George Massawe wakati akukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa tanki la maji katika kata ya Isengwa wilayani Meatu mkoa wa Simiyu leo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa RUWASA Meatu Mhandisi George Massawe mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa tanki la maji katika kata ya Isengwa wilayani Meatu mkoa wa Simiyu leo.
Mbunge wa jimbo la Meatu Leah Komanya mkoani Simiyu akizungumza katika mkutano na wananchi wa kata ya Nghoboko.
Wananchi mbalimbali wakisikiliza hotuba za viongozi waliohutubia mkutano huo wakiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakazi wa kijiji cha Sanga Itinje waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili wilayani Meatu mkoa wa Simiyu. (Picha na Adam H.Mzee/CCM Makao Makuu)
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akishiriki ujenzi wa katika Shule ya Sekondari Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoa wa Simiyu. (Picha na Adam H.Mzee/ CCM Makao Makuu).
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wakazi wa shina namba 1 Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoa wa Simiyu. (Picha na Adam H.Mzee/ CCM Makao Makuu).
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakazi waliojitokeza mara baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoa wa Simiyu. (Picha na Adam H.Mzee/ CCM Makao Makuu).
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akikagua maendeleo ya ujenzi wa katika Shule ya Sekondari Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoa wa Simiyu. (Picha na Adam H.Mzee/ CCM Makao Makuu).
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akihutubia wakazi waliojitokeza mara baada ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoa wa Simiyu. (Picha na Adam H.Mzee/ CCM Makao Makuu)
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ametoa wiki nne kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kushughulikia changamoto ya wanyama wakali wanaowasumbua wananchi wilayani Meatu.
Chongolo ameyasema hayo leo alipokuwa ziarani Wilaya ya Meatu katika kijiji cha Mwandu Itinje mkoani Simiyu wakati akziungumza na wana CCM katika shina namba 1 kijini hapo.
Amesema kuwepo kwa changamoto hiyo hadi sasa ni ishara kwamba watendaji husika wamekaidi au kudharau maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan
“Rais Samia aliagiza wizara ishughulikiesula hilo , nasikitika kuona leo miezi mitatu imepita naona changamoto hii inaendelea na malalamiko bado yapo,” Amesema Daniel Chongolo.
“Hatuwezi kuwa na watu wanaoagizwa na Rais juu ya kuchukua hatua hawafanyi wanakaa ofisini, hii inaleta matatizo kwa wananchi na inaonyesha dharau kwa aliyekuagiza,” ameongeza.
Amewahakikishia wananchi kuwa ndani ya wiki nne uongozi wa wizara hiyo utafika wilayani humo, kwa ajili ya kushughulikia chagamoto hizo za wananchi.
Ameongeza kuwa CCM haitaridhia kuona wananchi wanateseka ilhali kiliomba ridhaa ya kuwaongoza vyema wananchi wa Tanzania.
“Tukubaliane kama wapo tayari kufanya kazi wafanye kama hawapo wamruhusu Raia awape wengine waifanye kazi hiyo,” amesema Daniel Chongolo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. David Kafulila akizungumza katika kijiji cha Nghoboko baada ya kuungana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo katika ziara hiyo amesema asubuhi alichelewa kuungana na katibu mkuu huyo kwa sababu ya kukutana na watu wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa TANAPA ambao walifika leo ofisini kwake
“Leo wamekuja watu 10 kutoka wizara ya maliasili na utalii ili kukutana na mkuu wa mkoa kwa ajili ya kushughulikia suala la Tembo Meatu ambapo wiki hii Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA) itaanza kusambaza maaskari wa wanyamapori katika vijiji vya Meatu ili kuzuia na kukabiliana na Tembo wanaosumbua wananchi,” Amesema David Kafulila.