Home LOCAL IGP SIRRO AHIMIZA MATUMIZI YA MIFUMO YA KIELEKTRONIKI

IGP SIRRO AHIMIZA MATUMIZI YA MIFUMO YA KIELEKTRONIKI

08/06/2022  DODOMA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema serikali imeendelea kuhimiza makusanyo ya fedha za Umma yafanyike kwa kutumia mfumo wa kielektroniki ikiwa ni utaratibu wa kudhibiti upotevu wa fedha na kuongeza mapato.

IGP Sirro amesema hayo akiwa jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa vituo tiba vya Jeshi la Polisi ambapo kikao kazi hicho kitafanya tathimini ya utendaji kazi na kuibua mapungufu sambamba na kujadili changamoto mbalimbali kwa ajili ya kuleta tija mahala pa kazi.

Aidha, IGP Sirro ameongeza kuwa ni vyema hospitali za Jeshi hilo zikawa kimbilio la wananchi wote kwa kutoa huduma bora kwa wateja.

Naye Mkuu wa Kikosi cha Afya Nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Hussein Yahaya amesema kuwa, hadi sasa kuna jumla ya vituo tiba 36 nchini ambavyo vimeendelea kutoa huduma mbalimbali za kitabibu na kwamba licha ya kuhudumia afya za askari na familia zao lakini pia wameendelea kutoa huduma za afya kwa wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here