Home LOCAL HAIRUHUSIWI KUMRUDISHA MGONJWA NYUMBANI KWA KUKOSA PESA YA MATIBABU; WAZIRI UMMY MWALIMU

HAIRUHUSIWI KUMRUDISHA MGONJWA NYUMBANI KWA KUKOSA PESA YA MATIBABU; WAZIRI UMMY MWALIMU

Na.WAF-Dsm

Taasisi ya Saratani ya Ocean Road imetakiwa   kutomrudisha mgonjwa yeyote wa Saratani nyumbani kwa sababu ya kutokuwa na pesa za matibabu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya wakati akizindua bodi ya udhamini ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

“Ni vyema mgonjwa anayefika kwenye hospitali akapewa matibabu kwanza kisha tutaona namna ya kufanya”.

Aidha, Waziri Ummy ameahidi kuipatia taasisi hiyo kiasi cha shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya kununua mashine ya CT-SCAN ili kuboresha huduma za matibabu pamoja na kumpunguza foleni kwa wagonjwa

“Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatekeleza kwa vitendo na inatatua changamoto za wananchi na kuhakikisha huduma bora zinatolewa hapa hapa nchini.


Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here