Home BUSINESS GGML YATUMIA ZAIDI YA BILIONI 13 KUTEKELEZA MIRADI YA ELIMU HALMASHAURI YA...

GGML YATUMIA ZAIDI YA BILIONI 13 KUTEKELEZA MIRADI YA ELIMU HALMASHAURI YA MJI GEITA.

Na: Costantine James, Geita.

Katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya elimu ndani ya mkoa wa Geita Kampuni ya uchimbaji wa dhahabu iliyopo mkoani Geita, Geita Gold Mining Limited (GGML) imetumia zaidi ya bilioni 13 katika utekelezaji wa miradi  ya elimu ndani ya halmashauri ya mji Geita.

Hayo yamebainishwa na Meneja Mwandamizi anayeshughulikia ushirikiano katika mgodi wa GGML Bw. Manace Ndoroma amesema tangu mwaka 2018 hadi 2022 kampuni ya GGML kupitia fedha za wajibu wa kampuni kwa jamii (CSR) zilizotolewa na kampuni hiyo ndani ya halmashauri ya mji Geita imetumia zaidi ya bilioni 13 katika kutekeleza miradi ya elimu.

Amesema fedha hizo zimesaidia katika kukabiliana na changamoto ya Elimu ikiwemo uhaba wa madarasa , Madawati pamoja na Miundombinu mingine katika halmashauri ya maji Geita.

Manase amesema kupitia fedha hizo zimeleta matokeo chanya ambapo ni pamoja na ujenzi wa shule mpya ya sekondari ya Mkangara/Kanyala ambayo imetumia zaidi ya milioni 150,000,000 kutoka katika fedha zilizotolewa na mgodi huo. 

“Tunapenda jamii inayozunguka migodi tunayofanyia kazi ifaidike kutokana na shughuli za uchimbaji dhahabu.

Tumekuwa tukishirikiana vizuri na serikali kulipa kodi,tozo na fedha za wajibu wa kampuni kwa jamii kwa lengo la kuhakikisha uwepo wa kampuni yetu unakuwa na tija kwa jamii inayotuzunguka,”alisema Bwana Manace.

Mkuu wa shule ya Sekondari Mkangala Mwl. Egberth Kamugisha amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo umesaidia pakubwa kwa watoto wengi katika eneo kwani walilazimika kusafiri zaidi ya kilomita sita (6) hadi shule ya Sekondari Kasamwa.

“GGML na Halmashari wametusaidia katika ujenzi wa madarasa ambayo yalitusaidia mwaka 2021 kuwahamisha wanafunzi 220 waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kutoka eneo hili hadi Sekondari ya Kasamwa kwa ajili ya masomo.

Mwaka 2022 tumepokea wanafunzi wengine 212 wa kidato cha kwanza ambao sasa wanaifanya shule yetu iwe na jumla ya wanafunzi 432,”alisema Mwalimu Kamugisha.

Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya Mkangala wameupongeza mgodi huo kwa kuwezesha ujenzi wa shule hiyo hali iliyowawezesha kuepukana na kutembea umbali mrefu.

“Tulikuwa tukiwaona dada na kaka zetu wakiamka alfajiri sana kwenda kupata elimu katika shule ya Sekondari ya Kasamwa.Ujenzi wa shule hii mpya umeleta nafuu kubwa.

Ninaushukuru pia mradi wa shule hii kwa kuwa umetoa ajira kwa baba yangu mzazi ambaye amepata ajira ya muda mfupi kujenga shulehii.Hii inamsadia yeye kunilipia ada na kutupatia mahitaji muhimu ya kila siku,” amesema Elizabeth Mayala Mwanafunzi.

GGML imekuwa kinara wa uwekezaji kwenye jamii tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000 ambapo imekuwa na vipaumbele vikuu ikiwa nipamojan na kutekeleza miradi ya elimu, afya, maji, barabara.

Pamoja na miradi ya kukuza kipato na miradi mingine mingi ya kijamii ili kuhakikisha jamii mwenyeji inafaidika na uwepo wa mgodi wa GGML.

Mapema mwaka huu mgodi wa GGML uliibuka mshindi wa jumla katika kampuni zinazofanya vizuri kwenye sekta ya madini nchini Tanzania kwa mwaka wa fedha 2020/2021 baada ya kunyakua tuzo katika vipengele vya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii, mazingira, usalama, mlipaji bora wa mapato (kodi) na uendelezaji wazawa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here