Mkuu wa Wilaya ya Ubongo Kheri James (kulia) akikabidhi makusanyo kwa Mwenyekiti wa Chama kipya cha Umoja wa Wababa Kanisa la Anglicana Achidikonari ya Ubungo (UBAKI) Moses Manyatta (kushoto) yaliyokusanywa kutoka kwa washarika na waumini wa kanisa hilo (hawamo pichani) wakati wa sherehe za kuzindua rasmi Umoja huo zilizofanyika leo Juni 11,2022 katika kanisa la Mtakatifu Batolomayo Ubungo Jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM.
MKUU wa wilaya ya Ubungo Heri James amewataka viongozi wa Dini nchini kutumia nafasi zao kutoa elimu juu ya umuhimu wa sensa kwani kufanya hivyo kunatoa fursa kwa serikali kuwafikia wananchi wake kimaendeleo.
Amesema mwaka huu Agosti 23 ni mwaka wa sensa hivyo ni vema viongozi wakahamasisha wananchi wao na kuwakumbusha umuhimu wa kuhesabiwa ukizingatia zoezi hilo linafanyika kila baada ya miaka kumi.
James Ametoa kauli hiyo leo juni 11 mkoani Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa umoja wa Chama cha wababa (UBAK) wa Kanisa la Angalikana Archidikonary ya Ubungo uliofanyika katika la mtakatifu barthromayo wilayani humo.
“Kwanza nawapongeza kwa uzinduzi huu wa Chama cha wababa kwani kimekuja wakati sahihi ukizingatia mara zote tumekuwa na mambo ya akina mama tu hivyo Chama hiki ni sehemu ya juu kwa wababa katika kuwasilisha na kutoa maoni yao. Lakini pia tutumia umoja huu kukumbushana juu ya kulinda maadili yetu na malezi kwa vijana wetu.”amesema.
Nakuongeza kuwa “Serikali hususani Wilaya yangu ya Ubungo tuna mashirikiano mazuri na Kanisa la Angalikana kupitia viongozi wake, ni matumaini yangu hata katika hili la UBAKI tutaendelea kushirikiana pasipo shaka.
Pia amewahamisha waumini hao kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo wilayani humo hususani mikopo ambayo inatolewa bila riba kupitia halmashauri ya Ubungo,nakwamba wilaya hiyo ndio lango kuu la kuingilia mjini kati na hata stendi ya Magufuli ipo ubungo hivyo ni muhimu kuwa na jicho la kutazama fursa zilizopo za kiuchumi.
“Ndungu zangu kupitia Umoja huu tuimarishe malezi kwa vijana ,maadili ,na tuendelee kukemea wizi,ufisadi,dhuluma,ukatili na uhujumu kwani haya yote ni roho zisizokubarika katika jamii yetu“amesisitiza James.
kwa upande wake Kasisi Kiongozi wa kanisa la Angalikana Dayosisi ya Dar es Salaam Richard Kamenya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha UBAKI Moses Manyatta wamesema pamoja na mambo mengine yote lakinin pia watatumia umoja huo kuhamsisha waumini kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa linalotarajia kufanyika kitaifa Agosti 23 mwaka huu.
Pia wameipongeza na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuutoa kwenye Taasisi za dini hivyo wao kama viongozi jukumu lao kubwa ni kuendelea kusimamia utulivu uliopo.
katika uzinduzi huo wa Chama cha Umoja wa Baba UBAKI mkuu wa Wilaya hiyo ya Ubungo Heri James amechangia shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya kutunisha ufuko wa umoja huo.
Kwaya ya Umoja wa wakina Mama Kanisa la Anglicana Ubungo (UMAKI) wakitumbuiza.