Home LOCAL CHONGOLO ATOA ONYO KWA WATENDAJI WA CHAMA NA JUMUIYA WILAYA NA MIKOA...

CHONGOLO ATOA ONYO KWA WATENDAJI WA CHAMA NA JUMUIYA WILAYA NA MIKOA NCHINI

Katibu Mkuu ametoa onyo kwa makatibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kujihusisha na makundi ya wagombea katika uchaguzi unaoendelea ndani ya Chama na jumuiya zake.

Katibu Mkuu ameeleza hayo akiwa mgeni rasmi katika kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania Makao Makuu ya Chama Dodoma leo Jumatano tarehe 15 Juni, 2022.

“Nitoe Onyo kwa Makatibu wa Jumuiya, najua tangu mmeingia Dodoma mnazungushwa tu na wagombea, habari ninazo, kwa kuona, kwa ushahidi, na kila kitu mnazungushwa kutoka hoteli moja kwenda nyingine.”

Ndg. Chongolo amesistiza kuwa “Narudia natoa onyo kwa makatibu wote nchini, ninyi ni wakurugenzi wa uchaguzi, sitamani wala nisingependa kuona mnalichukulia suala hili la uchaguzi kishabiki kwa kutengeneza wagombea, nawaasa, kazi ni nzuri ukiikosa lakini ni mbaya sana ukiwa nayo.”

Na kwa bahati mbaya hao mnaowahangaikia hawana uwezo wa kuwarudisha kazini, siku moja kazi ukiikosa.

Previous articleMKUU WA MKOA WA RUVUMA AKABIDHI HATI KWA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA,AWATAKA WANA RUVUMA KUJIANDAA KUSOMA ELIMU YA JUU KUPITIA UWEKEZAJI UNAOFANYWA NA SERIKALI YA AWAMU YA SITA
Next articleTGNP, WADAU WATOA MAONI KUHUSU BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here