Home LOCAL CCM YAPONGEZA KASI YA SERIKALI KUTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI

CCM YAPONGEZA KASI YA SERIKALI KUTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Amosi Kanuda akiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Kamishna Msaidizi wa Polisi Advera Bulimba na viongozi wengine kukata utepe wa uzinduzi wa mradi wa maji uliotekelewa na serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWAS) Wilayani humo.

Na: Lucas Raphael,Tabora.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani hapa kimeipongeza serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kasi kubwa ya utekelezaji ilani ya uchaguzi katika sekta ya maji na nyinginezo.

Pongezi hizo zimetolewa na Viongozi wa Chama katika ziara maalumu ya uzinduzi wa miradi 13 ya maji iliyotekelezwa na serikali ya awamu ya 6 kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoani hapa kwa gharama ya shilingi bilioni  3.2.

Mwenyekiti wa CCM Wilayani Sikonge Anna Chambala na Katibu wake Magdalena Ndwete walisema kero ya maji katika Wilaya hiyo ilikuwa kubwa sana hali iliyopelekea kulalamikiwa na wananchi .

Walieleza kuridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya CCM katika kutatua kero hiyo ikiwemo kuwapatia fedha za kutosha Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa ajili ya utekelezaji miradi hiyo.

Ndwete alibainisha kuwa vijji vingi sasa vina miradi ya maji ambayo utekelezaji wake unaendelea na katika baadhi ya maeneo imekamilika na wananchi wanakunywa maji safi ya bomba, alitoa wito kwa jamii kutumia vizuri miradi hiyo.

Mwenyekiti wa CCM Wilayani Nzega Amos Kanuda alimpongeza Rais Samia kwa kuwapatia zaidi ya shilingi bilioni  9.4 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji katika vijiji zaidi ya 50 vilivyoko katika Majimbo ya Bukene na Nzega Vijijini.

Alibainisha kuwa licha ya maeneo mengi ya vijijini kuwa na shida kubwa ya maji, lakini juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya 6 zimeleta matumaini makubwa ya kumaliza kero hiyo katika vijiji vyote.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilayani Urambo Shaban Mussa aliipongeza juhudi zinazofanywa na Rais Samia katika kuhakikisha kero ya maji inabakia historia, alisema mkataba uliosainiwa hivi karibuni Ikulu kwa ajili ya kupeleka maji katika Miji 28 nchini ikiwemo Urambo ni faraja kubwa kwa wakazi wa wilya hiyo.

Viongozi wengine Mwenyekiti wa CCM Igunga Regina Thadeo na Katibu wa CCM Kaliua Salome Luhingulanya walimshukuru Rais Samia kwa kupeleka mabilioni ya fedha katika wilaya zao ili kutimiza azma yake ya kumtua mama ndoo kichwani.

Walimpongeza kwa weledi na ujasiri mkubwa wa kutafuta fedha ndani na nje ya nchi na kuzipeleka kwa wananchi ili kuhakikisha ilani ya uchaguzi ya chama inatekelezwa kwa vitendo katika sekta zote ikiwemo sekta ya maji.

Miradi hiyo imetekelezwa  katika kipindi cha mwaka mmoja tu tangu Rais Samia aingie madarakani serikali yake imetekeleza zaidi ya miradi 143 katika Wilaya 6 Mkoani hapa ambazo ni Urambo, Kaliua, Uyui, Nzega, Sikonge na Igunga kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni  44.5

Mwisho.

Previous articleMJADALA WA BIASHARA NA UWEKEZAJI BAINA YA TANZANIA NA UHOLANZI WAAZIMIA KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA NCHINI
Next articleKAMPENI YA SMAUJATA KUFIKA KILA ENEO LA MKOA WA SINGIGA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here