Home BUSINESS BRELA, FCC, SIDO KUIMARISHA USHIRIKIANO

BRELA, FCC, SIDO KUIMARISHA USHIRIKIANO

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) Bw. William Erio (kulia) akibadilishana nyaraka na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) Bw. Godfrey Nyaisa mara baada ya kusaini mkataba wa ushirikiano.

kurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) Bw. William Erio  na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) Bw. Godfrey Nyaisa wakisaini mikataba hiyo.

kurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) Bw. William Erio akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusaini mikataba hiyo. kulia ni Sylivesta Mpanduji Mkurugenzi Mkuu wa SIDO.

Baadhi ya watendaji wa Brela na FCC wakiwa katika hafla hiyo.

DAR ES SALAAM.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imesaini makubaliano ya ushirikiano na Tume ya  ushindani  (FCC), wakati huo huo  FCC ikisaini na  Shirika  la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), yenye lengo la kuboresha mazingira  uwekezaji nchini.

Akizungumza mara baada ya utiaji saini makubaliano ya ushirikiano huo Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa amesema BRELA  ipo tayari kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa mbalimbali pale zinapohitajika.

Bw. Nyaisa amesema kuwa ushirikiano wa taasisi hizo za Serikali ambazo zinawezesha biashara  utatoa fursa kwa wawekezaji kupata masoko ya uhakika huku bidhaa zao zikiwa zinatambulika na Mamlaka husika. 

“Ndugu wanahabari tunaomba muufahamishe Umma wa Watanzania na wawekezaji  kuwa utiaji saini huu  unalenga kufungua milango zaidi ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuondoa migongano ya hapa na pale ambayo inaweza kuchelewesha michakato ya urasimishaji wa biashara, hivyo  tunafanya haya kuhakikisha  wawekezaji wanakamilisha michakato ya ufanyaji Biashara kwa wakati,” amefafanua Bw. Nyaisa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu  wa FCC, Bw. William Erio amesema yanapotokea malalamiko ya mtu kutumia alama  ya biashara ya mwingine FCC huomba taarifa kutoka BRELA kwani ndiyo yenye dhamana ya kusajili majina ya biashara, kampuni na alama za biashara.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Profesa Sylvester Mpanduji amesema SIDO kama mlezi wa viwanda vidogo itahakikisha inatoa ushauri na kuhimiza wadau wanaopata mafunzo kurasimisha biashara zao BRELA, ili  kukidhi vigezo katika soko la ndani na nje ya nchi.

Utiaji saini makubaliano hayo yamefanyika tarehe 23 Juni, 2022 katika ofisi za FCC, Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Waziri mwenye dhamana ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, yanayozitaka Taasisi chini ya Wizara hiyo, kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuvutia wawekezaji na kufanya Tanzania kuendelea kuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji. ushirikiano na kupeana mbinu ikiwa ni pamoja na elimu juu ya namna ya kushughulikia changamoto hizo.

Ameongeza kuwa sasa taasisi hizo zitaendelea na kampeni ya kutoa elimu ya namna ya kuunganisha makampuni ili wawekezaji wawe na uelewa wa namna ya kuunganisha ili kutekeleza matakwa ya kisheria na kuepuka adhabu zinazoweza kuwapata endapo wataunganisha makampuni yao bili kufuata utaratibu.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) Bw. Godfrey Nyaisa amesema Migogoro ya kusajili alama za biashara ni mingi sana na unaweza usijue kwa sababu labda uko nje, lakini sisi ambao tuko katika maofisi tumekumbana na changamoto nyingi sana za wafanyabiashara kugombania alama za biashara.

Kikubwa hapa kuhusu ushirikiano huu ni kwamba kama wadau tulioungana kama Brela na FCC ni kuhakikisha tunafanya kazi hii pamoja kubwa tunaloenda kulifanya ni kutoa elimu zaidi kwa walaji ili waweze kuelewa na kuepuka makosa yasiyokuwa ya lazima kwa sababu ya kutojua sheria na utaratibu tu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here