NA: MWANFISHI WETU.
MWANAMITINDO nguli hapa nchin Ally Rehmtullah, ameshinda tuzo ya ‘Mbunifu bora wa kiume 2022’, katika tamasha la Ghana Merit Award lililofanyika June10 nchin Ghana.
Kabla ya kupata tuzo hiyo Ally Rehmtullah, amewahi kupata tuzo ya Mbunifu Bora wa mwaka 2019 katika tamasha la Swahili Fashion Week.
Akizungumza na ukurasa huu baada ya kupokea tuzo hiyo amesema anafurahi kuona ulimwengu unafatilia kazi yake na kuahidi kuendelea kufanya vizuri.
“Nina furaha kwa sababu malengo yangu ya kuonyesha uwezo wangu duniani yanazidi kufanikiwa siku hadi siku ni washukuru wandaaji wa tuzo hizi niwaombe waendelee kuandaa kwa sababu inatupatia motisha ya kufanya kazi nzuri kila kukicha,” anasema Ally Rehmtullah.
Aliongeza kuwa ataendelea kufanya kazi yake kwa bidii na kuwasaidia wabunifu wengine hususa wachanga ili kuibua vipaji vipya katika nchi yetu.
“Ili tuendelee kufanya vizuri kimataifa ni vyema kuibua vipaji vipya kwa sababu sisi tuna zeeka ndomana nimekuwa nikianzisha vipindi mbalimbli vya kutoa frusa kwa wabunifu chipukizi.”
Naye muwakilishi wa tamasha hilo Michael Lincoln, aliyekuja kukabidhi tuzo hizo amesema Tanzania ni moja ya nchi inayofanya vizuri katika tasnia ya mitindo barani Afrika.
“Tanzania ni nchi ambayo wabunifu wake wanafanya kazi nzuri ndiyo sababu utaona tuzo zaidi ya mbili zimekuja Tanzania nazote ni kutoka katika vipengele vikubwa.”