Home SPORTS YANGA YATUA SHINYANGA KUIWEKEA KAMBI SIMBA

YANGA YATUA SHINYANGA KUIWEKEA KAMBI SIMBA

Na: Mwandishi wetu.

Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga waiweka kambi Simba Shinyanga  kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho utaopigwa katika dimba la CCM Kirumba.

Katika mchezo huo wa hatua ya nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo mabingwa watetezi ni Simba walitwaa taji hilo walipocheza fainali na Yanga, Uwanja wa Lake Tanganyika kwa ushindi wa bao 1-0.

Hata hivyo Kikosi cha yanga Jana walitoka sare ya 1-1 dhidi ya biashara,huku Simba nae alitoka sare 1-1 dhdi ya Geita.

Leo Mei 25 kikosi cha Yanga kimeanza safari kuelekea Shinyanga ambapo kitaweka kambi kwa ajili ya mchezo wao ujao dhidi ya Simba.

Kwa upande wa Kocha msaidizi  wa Kikosi cha yanga Cedrick Kaze, amesema kuwa wanatambua mchezo wao ujao utakuwa ni mgumu ila watajitahidi kusaka ushindi.

“Tunajua kwamba mchezo wetu ujao utwakuwa ni wa nusu fainali dhidi ya Simba, tunawaheshimu wapinzani wetu na tutafanya maandalizi vizuri,”.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here