Home SPORTS WKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA SC YAITUNGUA ROVU SHOOTING 4-1 KWA MKAPA

WKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA SC YAITUNGUA ROVU SHOOTING 4-1 KWA MKAPA

Na: Mwandishi wetu, DAR.

Wekundu wa msimbazi timu ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ruvu Shooting Mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yamefungwa na Kibu Denis dakika ya 40,Larry Bwalya dakika ya 66,John Bocco dakika ya 81 na Henock Inoga dakika ya 84 na bao la kufutia machozi la Ruvu Shooting limefungwa na Haruna Chanongo dakika ya 82.

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 46 na kupunguza pengo la Pointi dhidi ya Yanga yenye Pointi 56 na kuwa tofauti ya Pointi 10 timu zote zikiwa zimecheza mechi 22 na kubakiwa na mechi 8 huku Ruvu wakishuka nafasi ya 14 wakiwa na Pointi 22.

Mchezo mwingine umepigwa uwanja wa Mkwakwani Tanga wenyeji Coastal Union wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania na kupanda hadi nafasi ya 12 ya Msimamo wa Ligi hiyo.

Ligi Kuu ya NBC itaendelea kesho kwa mchezo mmoja

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here