Home BUSINESS WAZIRI NAPE NNAUYE ATEMBELEA BANDA LA STAMICO MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU...

WAZIRI NAPE NNAUYE ATEMBELEA BANDA LA STAMICO MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI JIJINI ARUSHA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) akiwa katika Banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Madini Mchenjuaji wa Shirika la STAMICO Happy Mbenyange kuhusu shughuli wanazofanya leo Jumatatu Mei 2022 katika ukumbi wa Gran Melia Hotel Jijini Arusha. Waziri Nape Nnauye ametembelea banda la STAMICO wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti’. Picha na Kadama Malunde 1 blog
 Mhandisi wa Madini Mchenjuaji wa Shirika la STAMICO Happy Mbenyange akimwelezea Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (kulia) kuhusu Mkaa Mbadala uliopewa jina la Rafiki Briquettes unaotengenezwa kutokana na makaa ya mawe kutoka Mgodi wa Makaa ya Mawe STAMICO Kiwira – Kabulo mkoani Mbeya.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akiipongeza STAMICO kwa shughuli wanazofanya alipotembelea banda la STAMICO wakati akifungua maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani na Maonesho ya Kihabari yanayoambatana na Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani Jijini Arusha yakiongozwa na kauli mbiu ‘Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti’. Kulia ni Mhandisi wa Madini Mchenjuaji wa Shirika la STAMICO Happy Mbenyange.

Previous articleMAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA) YASHIRIKI SHEREHE ZA MEI MOSI DAR
Next articlePicha : NAPE NNAUYE AFUNGUA MAADHIMISHO SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI… ATEMBELEA BANDA LA MISA – TAN MAONESHO YA KIHABARI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here