Home ENTERTAINMENTS WASHIRIKI WA MISS TANZANIA 2022 WAFANYA ZIARA JAN INTERNATIONAL

WASHIRIKI WA MISS TANZANIA 2022 WAFANYA ZIARA JAN INTERNATIONAL

NA: MWANDISHI WETU.

WASHIRIKI wa shindano la Miss Tanzania 2022,  leo wametembelea moja ya wadhamini wao kampuni ya magari Jan international, iliyopo Namanga jijini Dar Es Salaam.

Kampuni hiyo inayoingiza na kuuza magari nchini, ndiyo iliyotoa gari  atakalo kabidhiwa mshindi wa kwanza aina ya Mercedes Benz yenye garama ya milioni 40 za kitanzania.

Akizungumza na wandishi wa habari katika ofisi hizo afisa masoko wa kampuni hiyo Basilisa Biseko alisema shindano la Miss Tanzaania linaibua wasichana wengi ambao wanafanya vizuri katika taifa ndio sababu wametoa zawadi yenye hadhi ya juu.

“Tumeliheshimisha shindano la Miss Tanzaania kwa kumpatia mrembo gari inayo endana na hadhi yake ili kutoa chachu kwa wasichan wengine kujitokeza kwa wingi na kutia jitihada kupeperusha bendera ya taifa letu katika tasnia ya urembo,” anasema Basilisa Biseko.

Aliongeza kuwa ndani ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa kampuni wamekuwa wakidhamini mashindano mbalimbali na kushiriki mamabo ya kijamii yanayo kwamua vijana kuishi katika ndoto zao.

Ikumbukwe kuwa mshindi atayepatikana kesho ndiye atakuwa muwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya urembo duniani akiwa chini ya kampuni ya The Look Campan Limited.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here