Home LOCAL WALIMU 332 WA MASOMO YA SAYANSI KIMU NA KILIMO WAJENGEWA UWEZO WA...

WALIMU 332 WA MASOMO YA SAYANSI KIMU NA KILIMO WAJENGEWA UWEZO WA KITALAAMU.

NA: FARIDA MANGUBE, MOROGORO. 
Waziri wa  Elimu Sayansi na Teknolojia  Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali imejipanga kufanya  mabadiliko makubwa katika sekta ya Elimu hapa nchi kuanzia Shule ya Msingi ikiwemo kuwaandaa wanafunzi kujifunza kwa vitendo masomo ya michepua ya Sayansi kimu na kilimoili  waweze kupata ujuzi wa  kukidhi matakwa ya ajira ikiwemo kwenye sekta ya Utalii hapa nchini.
 
Waziri Profesa Mkenda ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati akifungua mafunzo mafunzo maalumu kwa walimu 322 wa masomo ya Mchepuo wa kilimo na Sayansi kimu kutoka mikoa ya yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
 
Alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wameshaweka mikakati ya kuwandaa Walimu kwa kuwapa mafunzo ndani na nje ya nchi ili kuwafundisha wanafunzi.
 
Aidha  alisema tayari Wizara hiyo imeanza kutoa kipaumbele kwa mafunzo ya walimu wa masomo hayo hapa nchini kwa kuwaongezea ujuzi na maarifa ya kwenda kuwafundisha wanafunzi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
 
Lengo la mafunzo hayo ni kuandaa vijana ambao wataweza kuongeza ajira katika sekta ya kilimo na utalii ambao tayari umeshatangazwa nje ya nchi na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Filamu ya Utalii ya “ The RoyarTour.

Kwa Upande wake  wa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET),Dk Aneth Komba,alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kitalaamu walimu wa masomo ya Sayansi kimu na Kilimo kwa kuwapa mbinu za ufundishaji, ujifunzaji na upimaji unaozingatia ujenzi wa umahiri .

Dk Komba alisema kuwa matokeo ya mafunzo hayo yataweza kumuwezesha muhitimu wa masomo hayo kupata maarifa ,stadi za kutenda uelekeo wa kujitegemea kwa manufaa mapana ya jamii na Taifa kwa ujumla .
 
Alisema mafunzo ni ya kundi la tatu la walimu 322 ambao wanatoka katika shule za Serikali na Binafsi ili kuwajengea uwezo mkubwa wanafunzi ambao wataingia katika soko la ajira.
 
Naye  Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi,Hadija Mcheka,alisema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati kutokana na kuwepo kwa upungufu mkubwa wa walimu wa masomo hayo na kwamba wataendelea kushirikiana na wizara ya elimu kusaidia kuongeza idadi ya walimu.
 
Mafunzo hayo ya siku tano  yametolewa kwa waliu 332 kutoka shule za Serikali na binafsi  upande wa Tanzania bara na visiwani wanaofundisha  masomo ya kilimo na Sayansi kimu.

Mwisho
Previous articleVITUO VITATU VYA KUTOA HUDUMA ZA AFYA VYASITISHWA KUTOA HUDUMA MKOANI KAGERA
Next articleSIKU YA KWANZA KUELEKEA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA URITHI WA DUNIA – AFRIKA YAANZA KWA KISHINDO KILWA MASOKO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here