Home LOCAL VITUO VITATU VYA KUTOA HUDUMA ZA AFYA VYASITISHWA KUTOA HUDUMA MKOANI KAGERA

VITUO VITATU VYA KUTOA HUDUMA ZA AFYA VYASITISHWA KUTOA HUDUMA MKOANI KAGERA

Na.WAF-Kagera.

Vituo vitatu vya kutolea huduma za afya binafsi vimesitishwa kutoa huduma na vingine 25 vimepewa adhabu Mkoa Kagera kufuatia ukaguzi uliofanywa na Bodi ya hospitali binafsi.

Vituo hivyo binafsi  vimepata adhabu  kufuatia ukaguzi uliofanywa na Wizara ya Afya kupitia Bodi ya Ushauri ya Hospitali Binafsi.

Akiongea wakati wa kikao cha pamoja kati ya Bodi na wamiliki wa hospitali binafsi Msajili wa Bodi hiyo Dkt. Francis Mwanisi amesema  kati ya vituo 67 vilivyokaguliwa, vituo 25 sawa na asilimia 37.3 vimepewa adhabu  na vingine vitatu kusitishiwa huduma mpaka watakaporekebisha mapungufu yaliyobainisha

Dkt. Mwanisi amewataka wamiliki wa hospitali binafsi nchini kufuata sheria, kanuni na miongozo ya serikali  ili kutoa huduma za afya zenye ubora katika vituo vyao 

“Vituo vilivyo sitishiwa huduma vilikutwa na makosa yaliyoshindwa kuvumilika hii ni kusema kuwa bado vituo vingi havizingatii sheria, kanuni na miongozo vilivyosajiliwa nayo, hivyo nichukue fursa hii kuwataka wamiliki na watumishi wa hospitali binafsi kufuata sheria, kanuni na miongozo ili kutoa huduma bora kwa wananchi ” Amesema Dkt. Mwanisi.


Aidha,Dkt. Mwanisi amevitaka vituo binafsi vya Afya kutoa huduma kuendana na hali yao ya usajili na sio vinginevyo

“Baadhi ya vituo vinatoa huduma nje ya wigo wao wa usajili mfano; Zahanati kulaza wagonjwa zaidi ya masaa 24 na kuwa na vitanda vingi zaidi ya 40 vya kulaza wagonjwa Dkt.Mwanisi.

Vilevile Dkt. Mwanisi amewataka wamiliki wa hospitali binafsi kulipa mishahara ya watumishi wao kwa wakati ili waweze kutoa huduma kwa wagonjwa bila mawazo na kwa ufanisi wa hali ya juu.



“Mshahara ni haki ya mtumishi, Baadhi ya Wamiliki wa Vituo binafsi vya kutolea huduma za afya hawalipi Watumishi wao mishahara kwa wakati kwani wengine hadi miezi sita, sijui unategemea ataishije” Amesema Dkt. Mwanisi

Dkt. Mwanisi ameongeza kuwa katika ukaguzi huo bodi ya hospitali binafsi nchini imebaini udhaifu na changamoto mbali mbali zilizopo katika vituo hivyo ikiwa ni Baadhi ya Vituo kutumia dawa zilizoisha muda wake wa matumizi ambazo ni sumu na vingine kuwa na Miundombinu  mibovu ambayo inahatarisha Maisha ya Wagonjwa na Wafanyakazi kwa ujumla kwani baadhi ya majengo yana nyufa/

MWISHO

Previous articleMPANGO WA KUINUA UFAULU MASHULENI (PIP) WA BARRICK BULYANHULU WAZIDI KUPATA MAFANIKIO NYANG’HWALE
Next articleWALIMU 332 WA MASOMO YA SAYANSI KIMU NA KILIMO WAJENGEWA UWEZO WA KITALAAMU.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here