Home ENTERTAINMENTS UWT NJOMBE WASIFU UBORA WA FILAMU YA ‘ROYAL TOUR’

UWT NJOMBE WASIFU UBORA WA FILAMU YA ‘ROYAL TOUR’

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) Mkoa wa Njombe Scholastika Kevela ameisifu ubora wa filamu ya ‘Royal Tour’ na kudai kuwa watanzania wamepata jambo zuri la kuwatangaza Duniani.

Aidha amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha filamu hiyo ambayo ndani yake imeonyesha vivutio mbalimbali vya utalii na utamaduni wa watanzania huku Rais Samia akiwa ndiye mhusika mkuu wa filamu hiyo.

Mama Kevela ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kushiriki uzinduzi wa filamu hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) uliopo eneo la Posta Jijini Dar es Salaam.

“Ukweli filamu ni yenye viwango vya juu kabisa kwa waliobahatika kuitazama nadhani watakubaliana na mimi katika hili, haina shaka kuwa dunia itaitambua zaidi Tanzania kwa Sasa hasa vivutio vyake ilivyonavyo” amesema Mama Kevela

Aidha amesema matumaini take baada ya filamu hiyo kuonyeshwa katika nchi mbalimbali, idadi ya watalii wanaokuja nchini itaongezeka maradufu hivyo kuliwezesha Taifa kuvuna mapato ya kutosha kupitia sekta ya utalii.

Uzinduzi wa filamu hiyo umeudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu was Rais Dk Philip Mpango, Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mabalozi kutoka nchi mbalimbali waliopo nchini, Mawaziri, Mikoa, Viongozi wa Dini mbalimbali,Wakuu was Wilaya na viongozi na wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa.

Awali filamu hiyo ilizinduliwa Kwa mara ya kwanza katika Jiji la New York na Los Angeles Marekani ma baadae hapa nchini ilizinduliwa wiki iliyopita katika Jiji la Arusha na hapo na ilizinduliwa Zanzibar na kuudhuriwa viongozi mbalimbali.

Akizungumzia filamu hiyo Rais Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania kujivunia, huku wachambuzi mbalimbali wa masuala ya kiuchumi, kidiplomasia kisiasa wakiitaja hatua hiyo kuwa ni faida kwa namna mbalimbali kwa Tanzania.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here