Home BUSINESS UWEZO WA TANZANIA KUUZA MAZAO NA BIDHAA NJE UNAONGEZEKA: WAZIRI KIJAJI

UWEZO WA TANZANIA KUUZA MAZAO NA BIDHAA NJE UNAONGEZEKA: WAZIRI KIJAJI

BUNGENI DODOMA.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe.  Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema uwezo wa Tanzania kuuza nje mazao na bidhaa unaongezeka hususan uuzaji wa bidhaa zilizoongezwa thamani katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa. 

Pia matumizi ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi yameongezeka na hivyo kuchochea kupunguza uagizaji nje wa baadhi ya bidhaa na malighafi na hivyo kuiwezesha nchi kupunguza matumizi ya fedha za kigeni. 

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Mei 6, 2022 Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara kwa mwaka 2022/2023. 

Aidha, Dk Kijaji amesema mauzo ya bidhaa kwenye soko la China yaliongezeka kutoka dola za Marekani Milioni 238.9 mwaka 2020 hadi dola za Marekani milioni 273.1 mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 14.31. 

Amesema manunuzi ya Tanzania kutoka China yameongezeka kutoka dola za Marekani milioni 1,940.3 mwaka 2020 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 2,696.2 mwaka 2021, ikiwa ni pungufu kwa asilimia 38.94. 

Dkt. Kijaji alisema mauzo katika Soko la India yaliongezeka kutoka dola za Marekani milioni 528.7 mwaka 2020 hadi dola za Marekani milioni 1,008.7 mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 90.79.

 Aidha, Manunuzi ya Tanzania kutoka India yaliongezeka kutoka dola za Marekani milioni 1,940.3 mwaka 2020 hadi dola za Marekani milioni 2,696.2 mwaka 2021, ikiwa ni ongezeko la asilimia 38.96. Amesema Dkt. Kijaji. 

Dkt. Kijaji amesema mauzo katika soko la Japan yaliongezeka kutoka dola za Marekani milioni 55.8 mwaka 2020 hadi dola za Marekani milioni 67.5 mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 20.97. 

“Manunuzi ya bidhaa kutoka Japan yalikuwa na thamani ya dola za Marekani milioni 338.4 mwaka 2020 ikilinganiswa na dola za Marekani milioni 469 mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 38.59.” Amesema Dkt. Kijaji. 

Amesema bidhaa zilizonunuliwa na Tanzania kutoka Jumuiya ya Ulaya zilikuwa na thamani ya dola za Marekani milioni 1,072 mwaka 2020 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 1,003.7 kwa mwaka 2021, sawa na upungufu wa asilimia 6.37. 

Amesema mauzo ya bidhaa za Tanzania kwenda Jumuiya ya Ulaya yalipungua kutoka dola za Marekani milioni 1,475. kwa mwaka 2020 hadi kufikia dola za Marekani milioni 857.1 mwaka 2021, ambayo ni sawa na upungufu wa asilimia 41.89. 

Amesema mauzo ya Tanzania katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2021 yalikuwa dola za Marekani milioni1, 161.2 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 807.9 mwaka 2020 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 43.73. 

Kwa upande mwingine, uagizaji wa Tanzania kutoka nchi za Jumuiya hiyo uliongezeka kutoka dola za Marekani milioni 324.3 mwaka 2020 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 523.4 mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 61.39. Kutokana na hali hiyo, urari wa biashara ni chanya kwa dola za Marekani milioni 637.8. Amesema Dkt. Kijaji. 

Amesema mauzo ya Tanzania kwenda katika soko la nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, mwaka 2020 yalikuwa dola za Marekani milioni 1,458.3 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni1 311.5 mwaka 2021, sawa na upungufu wa asilimia 10.06. 

Dkt. Kijaji pia amesema uagizaji wa Tanzania kutoka katika soko hilo ulipungua kutoka dola za Marekani milioni 492.4 mwaka 2020 hadi dola za Marekani milioni 232.5 mwaka 2021, sawa na upungufu wa asilimia 52.78.

(mwisho).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here