Home LOCAL UPATIKANAJI WA MAJI MJINI GEITA WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 4

UPATIKANAJI WA MAJI MJINI GEITA WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 4

Na: Costantine James, Geita.

Mkuu wa mkoa wa Geita mhe, Rosemary Senyamule amewataka wakazi wa mkoa wa Geita  kuitunza na kuilinda miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayotekelezwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ndani ya mkoa huo.

Amebainisha hayo leo 31.5.2022 alipotembelea miradi ya maji katika eneo la Igembe Nsabo pamoja na Chankolongo ndani ya halmashauri ya mji Geita amesema serikali imetoa milioni 511 kupitia mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mjini Geita (GEUWASA) kwa lengo la kutekeleza miradi ya maji ndani ya halmashauri hiyo.

Amesema ujenzi wa miardi ya maji kupitia Fedha za mpango wa maendeleo na ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 zimesaidia ongezeko la upatikanaji wa maji mjini Geita kwa asilimia 4 hivyo kuwezesha kufikia asilmia 75 ya upatikanaji wa maji mjini Geita.

Mhe, Senyamule amesema jukumu la kulinda na kutunza miradi ya maendeleo ni jukjumu la kila mtu ili kuwezesha miradi  hiyo kutumika kwa mada mrefu zaidi kama ilivyo kusudiwa.

Senyamule amewapongeza GEUWASA kwa kukamilisha miradi ya maji mjini Geita kwa wakati hali iliyopelekea kuongezeka kwa  upatikanaji wa maji mjini Geita kutoka asilimia 71 hadi kufikia asilimia75  hata hivyo amewataka viongozi mbali mbali wanaosimamia miradi ya kimaendeleo ndani ya mkoa  wa Geita  kuhakikisha inakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake meneja wa GEUWASA mjini Geita Mhandisi Frank Changawa ameipongeza serikali kwa kutoa fedha kiasi cha milioni 511 ambazo zimesaidia kujenga miradi ya maji pamoja na kupanua wigo wa upatikanaji wa maji mjini Geita.

Mhandisi Changawa amesema mamlaka ya maji mjini Geita GEUWASA imejipanga kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji mjini Geita kwa kusimamia mradi wa  kupanua chujio la maji unaoendelea kujengwa katika eneo la nyankanga mjini Geita.

Amesema mradi huo utakapo kamilika utaongeza uzalishaji wa maji kutoka lita milioni 3 hadi lita milioni 7  mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 25% na pindi utakapo kamilika utasaidia kuimalika kwa huduma ya maji mjini Geita.

Baadhi ya wakazi wa halmashauri ya mji wa Geita wameipongeza serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa miradi mbalimbali ya maji mjini Geita.

Wamesema kukamilika kwa miradi ya maji Mjini Geita kutasaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa maji kutokana na kuwa na changamoto ya ukosefu wa maji kwa mda mrefu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here