Home BUSINESS UFARANSA YAZINDUA MRADI WA ‘Innoversity’ KUWAWEZESHA WABUNIFU NA WAJASIRIAMALI KATIKA VYUO VIKUU...

UFARANSA YAZINDUA MRADI WA ‘Innoversity’ KUWAWEZESHA WABUNIFU NA WAJASIRIAMALI KATIKA VYUO VIKUU VITATU TANZANIA

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawamo pichani) kuhusu ufadhili wa Mradi wa miaka miwili wa ‘Innoversity’ katika makazi yake leo Mei 24, 2022 Jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari (hawamo pichani) leo Mei 24, 2022 Jijini Dar es Salaam. (kushoto) ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Samson Mwela, na (kulia) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Sahara Ventures Jumanne Mtambalike.

Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Samson Mwela (kushoto) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawamo pichani) alipokuwa akielezea juu ya Mradi huo, Jijini Dar es Salaam. (kulia) Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui

Afisa Mtendaji Mkuu wa Sahara Ventures Jumanne Mtambalike (katikati) akizungumza katika mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam. (kulia) ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui, na (kushoto) ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Samson Mwela.


Mkuu wa Ushirikiano na Utamaduni wa Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania Cecil FROBERT (kulia) akizungumza alipokuwa akimkabiribisha Balozi Nabil Hajlaoui kuzungumza kwenye Mkutano huo. (kushoto) ni Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui.


Afisa habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Ufaransa Iku Kasege (kulia) akiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Beatrice Shayo wakimsikiliza Balozi Hajlaoui (hayumo pichani) alipokuwa akizungumza kwenye mkutano huo leo Mei 24, 2022 Jijini Dar es Salaam.



Picha za waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika mkutano huo. PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO.



Picha ya pamoja

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.
 

Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania umetoa ufadhili wa miaka miwili wenye thamani ya Euro 570,000 sawa  na Shilingi Billioni 1.5 za Tanzania kwa wabunifu na wajasiriamali katika mradi wa  ‘Innoversity’ unaotekelezwa katika vyuo vikuu vitatu  vya Tanzania Bara chini ya usimamizi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na  kampuni ya Sahara Ventures wataalam wa biashara na kilimo.

Akizungumza leo Mei 24, 2022 Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua rasmi mradi huo, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui amesema kuwa kuzinduliwa kwa mradi huo ni jitihada za kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuvipa vyuo vikuu maarifa, zana na rasilimali za kukuza ubunifu, ujuzi wa kujiajiri na ujasiriamali na kwamba ufaransa inaamini kuwa kuwepo kwa mradi huo kutaleta matokeo chanya  kwa Tanzania na nchi nyingine za Afrika.

”Licha ya kudumisha mahusiano bora yaliyopo baina ya Ufaransa na Tanzania pia tunatambua jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika masuala ya ujasiriamali na uvumbuzi na hata alipotembelea Paris alitembelea sehemu nyingi na kuzungumza namna ya kuleta ujuzi hapa nchini kwa manufaa ya watanzania hasa vijana.” Amesema Balozi Hajlaoui.

Balozi Hajlaoui ameongeza kuwa mradi huo  unatekelezwa katika vyuo vikuu vitatu ambavyo ni Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (Arusha,) Chuo kikuu cha Sokoine (SUA,) na Chuo Kikuu cha Iringa (UoI) kwa lengo la kuimarisha Taasisi hizo kama nyenzo muhimu za elimu ya juu Tanzania, sambamba na kusaidia kukuza ujasiriamali kwa wanafunzi wa Taasisi hizo pamoja  na kukuza ajira.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Samson Mwela  ameishukuru Serikali ya Ufaransa kwa kuendeleza ushirikiano wenye tija na Tanzania na kuahidi ushirikiano katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa asilimia 100.
 
Amesema kuwa mradi huo wenye lengo la kuwawezesha wabunifu na wajasiriamali umeweka mkazo katika sekta ya kilimo na ujasiriamali kwa vijana wa vyuo vikuu ili kutatua changamoto ya ajira.
 
”Mradi huu utanufaisha zaidi ya wanafunzi vijana 300 pamoja na wahadhiri na watafiti kutoka vyuo vikuu vitatu Tanzania, huu ni mradi wa kihistoria kwa kuwa kutakuwa na ubadilishanaji wa ujuzi kwa watanzania kwenda Ufaransa na vijana wa Ufaransa kuja Tanzania kujifunza zaidi.” Amesema.
 
Na kuongeza kuwa ”Serikali inatoa fedha nyingi kusaidia tafiti na bunifu kupitia COSTECH, mwaka huu imetoa bilioni 3.5 na mwakani tunategemea kupokea bilioni 5 zaidi niwatake vijana na wabunifu kutoka vyuo nufaika vya mradi huu wajitokeze kupitia mradi huu na miradi mingine mingi inayosimamiwa na COSTECH.” Ameongeza.
 
Mwisho.
 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here