Home LOCAL TUZO NONO ZA TMDA CHACHU KWA WANAHABARI NCHINI

TUZO NONO ZA TMDA CHACHU KWA WANAHABARI NCHINI

MNAMO wa Aprili 27, mwaka huu, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),ilitoa tuzo kwa Waandishi wa habari Watano, kwa mara ya kwanza toka TMDA ianze.

Washindi walipatiwa Trophy na pesa Taslim TZS. 1,000,000/=

Hii ni hatua kubwa kwa TMDA kuthamini mchango na kazi ya waandishi wa habari.

Kwa mara nyingine tunawapongeza washindi wote Veronica Mrema @⁨Veronica Mrema⁩ , Avelyne Kitomari , Andrew Chale na Waziri Suka.

Tuzo hizi nono ziende kuwa chachu kwa Wanahabari wengi zaidi katika kujikita kuandika na kuhabarisha Umma habari za udhibiti wa dawa, Vifaa tiba na bidhaa za tumbaku, shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo.

Hii ni bahati ya kipekee kwa thamani ya tuzo hizi nono kwani zimeweza kuwa kielelezo kwa Wanahabari wengi licha ya kutolewa kwa mara ya kwanza.

Kila lakheri TMDA kuelekea mwezi Julai 2022, ambapo inaenda kutimiza miaka 19 ya uwepo wake tangu ianze.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here