Home LOCAL TANZANIA YALIPONGEZA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO)

TANZANIA YALIPONGEZA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO)

Na.WAF-Geneva.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelipongeza shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kutoa usaidizi wa kitaalamu na misaada ya kibinadamu katika kukabiliana na magonjwa.

Pongezi hizo zimetolewa na Dkt. Catherine Joachim  wakati wa mkutano wa 75 wa Shirika Afya Duniani.

Dkt.Catherine amesema shirika hilo limepata mafanikio baada ya kuwa bega kwa bega na nchi wanachama katika kudhibiti athari za UVIKO-19. 

“Shirika la Afya Duniani (WHO) haliwezi kufikia malengo iliyojiwekea bila ya kuwa na vyanzo vya fedha vilivyo endelevu katika kuendesha programu za Afya Duniani. “Amesema Dkt. Catherine 

Aidha, amesema kikosi kazi cha wataalamu cha masuala ya ugharimishaji wa shirika hilo wamependekeza kuona umuhimu wa nchi wanachama kuongeza michango. 

Hata hivyo wamesema mkakati wa kuongeza michango uende sambamba na kuimarisha uwajibikaji wenye tija na uwazi katika matumizi ya fedha za shirika hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here