Home Uncategorized SIMBA YATINGA NUSU FAINALI YA KOMBE LA AZAM

SIMBA YATINGA NUSU FAINALI YA KOMBE LA AZAM

Na: Stella Kessy.

MABINGWA watetezi Simba leo wametinga nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Azam Sport Federation (ASFC kwa  kuichapa mabao 4-0 Timu ya Pamba FC kutoka Mwanza Mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mtanange huo Simba walionekana kutawala mchezo na bao la kwanza lilifungwa na  Peter Banda dakika ya 45 kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi ya Rally Bwalya bao ambalo lilidumu katika kipindi cha kwanza.

Huku katika Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko huku Simba ikinufaika zaidi na mabadiliko hayo.

Hata hivyo katika dakika ya 47  Kibu Denis aliwanyanyua mashabiki wa Simba  baada ya kupokea krosi ya Mohamed Hussein,na mabao mawili walitupiwa nyavuni na  Yusuph Mhilu dakika ya 52 na 88.

Kwa ushindi huo Simba watakutana na Yanga Nusu Fainali ya Michuano hiyo huku Azam FC watakutana na Coastal Union.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here