Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani wa Geita Kamishina Msaidizi Henry Mwaibambe amewataka Wazazi na walezi mkoani Geita kuhakikisha wanasimamia kikamilifu swala la ulinzi na usalama wa mtoto Mkoani humo ili kuhakikisha mtoto anakuwa salama.
Amesema hayo wakati wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake baada ya tukio la Mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Nyanza iliyopo halmashauri ya mji Geita Happines Mdoshi 15, alielazimika kukosa kufanya mitihani ya Pre- mock, baada ya kumwagiwa maji ya moto eneo la mgogoni pamoja na makalioni wakati wa kusherekea siku ya kuzaliwa kwake.
Tukio hilo limetokea wilayani Geita wakati binti huyo alipokuwa akisherekea siku yake ya kuzaliwa mtototo mwenzie akamumwagia maji ya moto hali iliyosababisha kushindwa kuhudhulia mitihani ya pre-mock ya kidato cha pili.
Kamanda Mwaibambe amewataka wazazi na walezi mkoani Geita kuwa kipaumbele katikakuhakikisha wanasimamia na kulinda ulinzi na usalama wa mtoto.
Wazazi wa watoto huyo wameeleza kuchukizwa na tukio hilo liliosabisha kuhatarisha afya na kumkosesha kufanya mitihani mtoto wao huku wakiwataka watu wengine kuachana na na mtimdo wa kusherekea siku ya kuzaliwa kwa kumwagiana maji.
Naye Mkuu wa wilaya ya Geita Wilson Shimo wamekiri kutokea kwa tukio hilo huku wakiwataka wazazi na walezi wilayani Geita kuwa waangalifu kwenye malezi na michezo hatarishi kwa usalama wa watoto.
Jamii ya sasa imekuwa na utaratibu wa kumtakia mtu heri ya kuzaliwa kwa kummwagia Maji na kumuimbia, lakini kwa binti Happy imekuwa tofauti baada ya kumwagiwa maji ya moto yaliyosababisha kushindwa Kufanya mtihani.
MWISHO.