Home SPORTS NABI, PABLO WATAMBIANA

NABI, PABLO WATAMBIANA

Na: Stella Kessy.

KOCHA Mkuu wa kikosi cha Yanga, Nassredine Nabi, amesema kesho hawata waachia simba nafasi ya kutinga fainali kwani msimu huu malengo yao ni ubingwa wa Kombe la Shirukisho la Azam ( ASFC) .

Yanga wanashuka katika dimba la CCM Kirumba saa Tisa Alasiri, kuvaana na mabingwa watetezi wakombe hilo Wekundu wa Msimbazi Simba SC.

Watani wajadi hao kwa msimu huu walikutana mara ya mwisho Mei 30 katika mchezo wa Ligi Kuu nakushindwa kuonuonyeshana umwamba kwakumaliza mchezo huo kwa suluhu kwenye Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na Leo na wanahabari  katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Gold Crest Mkoani Mwanza, Kocha Nabi amesema kuwa kesho  hawata bweteka katika kulipambania nafasi ya kutinga fainali ya ASFC.

Amesema mchezo huo nitofauti kabisa namchezo wa ligi hivyo wataingia kwa tahadhari na malengo yao yakiwa nikuwafunga wapinzani wao.

“Tutaingia Kwa tahadhari maana mchezo huu nitofauti nawaligi kwahiyo nia namalengo yetu nikupata ushindi mechi hii ndio funguo ya kwenda fainali lazima tupambane, “ alisema.

Kwa upande wake kocha wa simba Pablo Martin, alisema Yanga wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo lakini yeye amejipanga na baadhi yawachezaji wake ambao walikuwa maheruhi wamerudi nawatajiunga nakikosi kesho.

Alisema hawezi kuwataja wachezaji hao kwani atakuwa anataja silaha kwa maadui lakini mchezo utakuwa mgumu nawatajitahidi kupambana kutimiza malengo yao waliyojiwekea.

“Mchezo nimgumu na Yanga wanaonekana kama wana nafasi kubwa yakushinda lakini sisi tupo kamili natutajitahidi tuweze kuingia katika fainali kuutetea ubingwa, ” alisema 


Previous articleWILAYA YA IKUNGI NI SALAMA KWA WAFUGAJI NA WAKULIMA
Next articleBRELA YAKUSUDIA KUFUTA MAKAMPUNI 5,676
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here