Home BUSINESS MHE. MASANJA AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA WAHIFADHI

MHE. MASANJA AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA WAHIFADHI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka wananchi kushirikiana na askari wa uhifadhi ili kutunza maeneo yaliyohifadhiwa kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Ameyasema hayo hivi karibuni  katika ziara ya Mawaziri wa Kisekta ya kutatua migogoro ya ardhi katika ukumbi wa Benki Kuu Mkoani Mbeya.

“Tushirikiane kwa pamoja kutunza uhifadhi ili na wenyewe ututunze” Mhe. Masanja amesisitiza.

Amefafanua kuwa ni vyema wananchi wakaacha dhana ya kuwachukulia askari uhifadhi kama maadui na badala yake kushirikiana nao katika uhifadhi kwa maslahi ya Taifa.

Aidha , amewataka viongozi mkoani Mbeya kushirikiana kwa karibu na askari wa uhifadhi ili kulinda maeneo yaliyohifadhiwa pamoja na kuwaelimisha wananchi kwamba askari uhifadhi sio maadui wa wananchi.

Ametaja faida za kutunza maeneo yaliyohifadhiwa kuwa ni pamoja na kuhifadhi mazingira, kutunza vyanzo vya maji na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Ameongeza kuwa maeneo yaliyohifadhiwa yanategemeana na Sekta karibia zote akitolea mfano wa Sekta ya Maji, Sekta ya Uwekezaji na Mazingira.

Previous articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO JUMATATU MEI 9-2022
Next articleWAZIRI MKUU AFANYA ZIARA BOHARI YA DAWA (MSD)
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here