Home Uncategorized MFAUME MFAUME KUVUNJA UKIMNYA WA MWAKA MMOJA NA NUSU JUNE 10 JIJINI...

MFAUME MFAUME KUVUNJA UKIMNYA WA MWAKA MMOJA NA NUSU JUNE 10 JIJINI DAR ES SALAAM.


NA: MWANDISHI WETU.

BONDIA wa Ngumi za kulipwa nchini, Mfaume Mfaume, ameahidi wadau wa mchezo huo kufanya vizuri katika pambano la ”The Return of Nakoz King” dhidi ya Abdumonem Said, kutoka nchi ya  Misri.

 Pambano hilo la kuwania mkanda wa Ubingwa wa WBF lenye raundi 10 uzani wa kilo  69 litakalofanyika Juni 10, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam Jana, Mfaume alisema atafanya vizuri katika mchuano huo na kuahidi kumshushia kipigo kikali hasimu wake Abdumonem Said.

“Nimejiandaa vizuri sina wasi wasi maana nimekaa nje ya ulingo zaidi ya mwaka moja na miezi sita, nitaonyesha mchezo mzuri niwaombe mashabiki zangu kujitokeza kwa wingi siku hiyo kushuhudia nikipata mkanda wa WBF, “ anasema  Mfaume Mfaume.

Aidha alisema anatarajia kuanza Kambi hivi karibuni Kwa ajili kujiandaa kikamilifu chini ya Kocha wake, Rama Jah.

Kwa upande wa kocha wa bondia huyo,  Raha Jah alisema atahakikisha anamundaa vyema bondia wake ili kuonyesha mchezo nzuri siku hiyo.

“Tutaingia kambini kwa ajili ya  kujinoa kikamlifu nina mbinu kabambe za kumpa bondia wangu pamoja na  silaha kali kwa lengo la kubakisha mkanda huo unabaki nyumbani.”

Muandaaji wa pambano hilo  Siah Mosha alisema wadau wajitokeze kwa wingi kwa sababu mchuano huo ni mkubwa kutokana na uzito wa mabondia ambao wanacheza na historia zao ni nzuri.

“Nawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi katika pambano hili,  kwani viingilio vitatangazwa hivi karibuni ili wadau na wa mchezo huu wajitokeze siku hiyo, “ anasema Siah Mosha.

Aliongeza kuwa kutakuwa na mapambano  manne yatakayo chezwa na bondia Oscar Oscar atazichapa na Hassan Milanzi kutoka Zimbambwe, Juma Choki akichuana na Issa Nampepeche kwa ajili ya kuwania mikanda ya PST na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC).

Wengine ni Stumai Muki akipepechana na Chimwemwe Banda na Hasimi Maya atapigana na Mudochee Katembo kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here