Home ENTERTAINMENTS MCHENGERWA MGENI RASMI ADORABLE WEDDING TRADE FAIR MSIMU WA TANO

MCHENGERWA MGENI RASMI ADORABLE WEDDING TRADE FAIR MSIMU WA TANO

NA: MWANDISHI WETU.

MSIMU wa tano wa onyesho la Adorable Wedding Trade Fair, unatarajiwa kuanza mei 13 mpaka 15 katika ukumbi wa Mliman City jijini Dar Es Salaam.

Tamasha hilo linafanyika kwa mwaka mara moja kukutanisha watoa huduma mbalimbli katika hafla tofauti kukutana na wateja wao kuonana kazi zao.

Akizungumza na ukurasa huu muasisi wa onyesho hilo Anna Lema, amesema mwaka huu mgeni rasm katika maoshenyesho hayo atakuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa.

“Mwaka huu tumepata bahati ya kuwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo katika tamasha letu atakuja kutembelea  mabanda kuona kazi zetu na kuzungumza nasi changamoto tunazopitia hii itakuwa siku ya Mei 15, ambapo ndipo tutakuwa tukifunga tamasha letu,” anasema Anna Lema.

Aliongeza kuwa mpaka sasa tayari watoa huduma za sherehe mbalimbli zaidi ya mia moja wamesha fanya usahili wa kudhibitisha uwepo wao katika ukumbi wa Mlimani City.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here