Home ENTERTAINMENTS KWAYA YA GETHSEMANE WATOA VIDEO MPYA YA WIMBO WA BADO...

KWAYA YA GETHSEMANE WATOA VIDEO MPYA YA WIMBO WA BADO KITAMBO

Na:Mwandishi Wetu.

KWAYA maarufu nchini ya  Gethsemane Group Kinondoni (GGK) SDA wilayani Kinondoni mkoani Dar es Salaam wametoa  video mpya ya wimbo ujulikanao kama Bado Kitambo. 

Kwaya hiyo imejizolea umaarifu kutokana na mstari wa mbele kufariji taifa hususa ni pale walipotunga wimbo maalumu baada ya ajali ya meli ya MV. Nyerere na hata taifa lilipo ondokewa na aliyekua Raisi wa awamu ya tano Dk. John Magufuli, Gethsemane walikua moja ya kikundi cha uimbaji cha mwanzo kabisa ambao walitoa wimbo wa Faraja Kwa taifa. Wimbo ambao ulipokelewa vizuri sana Kwenye Jamii pamoja na vyombo Vya Habari.

Kwa mujibu wa uongozi wa kundi hilo umesema leo jijini Dar es Salaam kuwa baada ya kutoa video mbalimbali na kupokelewa vyema, kwa sasa wametoa video mpya ya wimbo uliopewa jina Bado Kitambo ambao ni mahususi katika kuwakumbusha  wanadamu kuwa  duniani tunapita.

Ila pamoja na  changamoto zote za dunia, ipo ahadi kwamba kuna Tumaini jipya Kwa wale washindi wa dhambi. Tuna imani kwamba wimbo huu utandelea kubariki watu wa imani na dini  zote na kuendelea kumtumaini Mungu na kushinda dhambi”

Uongozi wa Gethsemane umefafanua zaidi kwamba wimbo huo utakuwepo kwenye album yao mpya inayotarajiwa kutoka mwaka huu. “Tumeona wakati tunaendelea kurekodi album ambayo itakua na Nyimbo kumi, basi tuwape mashabiki wetu kionjo kidogo waendelee kubarikiwa wakati sisi bado tukiendelea na kurekodi. Tuna imani album Hii itakua mbaraka Kwenye Jamii. Wimbo wa bado kitambo unapatikana Kwenye Chanel yetu ya YouTube.”

Mwisho

Previous articleABSA BANK TANZANIA PROFIT AFTER TAX SOARS 155% IN THE FIRST QUARTER OF 2022
Next articleBASHUNGWA ATAKA LESENI ZA BIASHARA KUNDI A NA B KUTOLEWA SEHEMU MOJA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here