Home SPORTS KMC FITI KUIKABILI MBEYA CITY KESHO UHURU

KMC FITI KUIKABILI MBEYA CITY KESHO UHURU

 

NA: STELLA KESSY.

Kikosi cha KMC FC kesho kitashuka katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania bara dhidi ya Mbeya City utakaopigwa saa 16:00 jioni.

Kikosi hicho kikiwa chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana itakuwa nyumbani ikimkaribisha Mbeya City huku  maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa asilimia kubwa na hivyo Timu ipotayari kwa mtange huo.

Akizungumza na blog hii Afisa Habari na Mawasiliano KMC FC Christina Mwagala amesema kuwa  KMC imejipanga vizuri kutumia uwanja wanyumbani ilikupata matokeo mazuri na hivyo  kuendelea kujiimarisha zaidi kwenye msimamo wa Ligi kuu ya NBC ambapo kwa sasa ipo katika nafasi ya nane.

Aidha katika mchezo huo wa kesho KMC itakosa huduma ya wachezaji wawili ambao ni Nickson Kibabage kutokana na mambo ya kifamilia pamoja na Charles Ilamfya mwenye kadi tatu za njano.

Kwaupande wa Afya za wachezaji ziko vizuri ,wanahari na morali nzuri na kwamba wachezaji pamoja na benchi la ufundi wamejiandaa kuwapa burudani mashabiki na Watanzania wote ambao siku zote wamekuwa wakiisapoti katika hali yoyote pindi inapokuwa uwanjani.

“Tunakwenda kwenye mechi ngumu pamoja na kwamba tutakuwa nyumbani ,tunaiheshimu Mbye City kwakuwa ni wazuri, wanawachezaji wazuri, lakini KMC tukobora zaidi kuhakikisha alama tatu muhimu zinabaki kwenye Manispaa yetu ya Kinondoni.

Hata hivyo katika mchezo uliopita duru ya kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, timu zote mbili zilitoka zare ya mabao mawili kwa mawili ambapo magoli ya KMC yalifungwa na Matheo Anton pamoja na Mohamed Samata.

Previous articlePicha : RC SOPHIA MJEMA AZINDUA CHANJO YA UGONJWA WA KUPOOZA ‘POLIO’ MKOA WA SHINYANGA…WATOTO 450,000 KUPEWA MATONE
Next articleMWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) RAIS SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KAMATIYA SIASA MKOA WA TABORA LEO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here