Home Uncategorized KMC FC KUWAKARIBISHA MTIBWA SUGAR UWANJA WA UHURU KESHO

KMC FC KUWAKARIBISHA MTIBWA SUGAR UWANJA WA UHURU KESHO

Na: Stella Kessy.

Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kesho itakuwa nyumbani ikimkaribisha Mtibwa Sugar katika Dimba la Uhuru Jijini Dar  es Salaam kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania bara utakaopigwa saa nane kamili mchana (14:00).

Akizungumza na blog hii Afisa Habari na Mawasiliano wa KMC FC Christina Mwagala

Amesema kuwa kikosi chake kimefanya  maandalizi yake ya mwisho  leo ya kuwakabili Mtibwa Sugar ya Turiani Mkoani Morogoro na kwamba kikosi kiko tayari kwa mtanange huo.

Katika mchezo huo ambao KMC ni mwenyeji wamekuwa na wakati mzuri wakufanya maandalizi na kwamba licha ya kuwa mchezo utakuwa na ushindani mkubwa lakini kama Timu imejidhatiti kupata alama tatu muhimu.

“Tunakwenda kucheza na Mtibwa Sugar ,tunafahamu kuwa ni Timu nzuri na imekuwa na wakati mzuri kwenye michezo yake hivi karibuni, lakini KMC inawachezaji wazuri na bora ambao sikuzote wamekuwa tayari kuipambania Manispaa ya Kinondoni ipate matokeomazuri hivyo mashabiki msiwe na wasiwasi Timu ipo imara kwenye mchezo huo.”

“Michezo yetu hivi karibuni hatujapata matokeo rafiki,lakini tunawaahidi mashabiki zetu kufanya vizuri kwenye michezo inayokuja na kwa kuanza tunakwenda kupambana uwanjani katika mchezo wa kesho, hivyo kikubwa wazidi kuwasapoti wachezaji kwakuja uwanjani.

KMC hadi sasa imecheza michezo 22 ya ligi Kuu ya NBC na kukusanya jumla ya alama 24, nakuwa kwenye nafasi ya 11 na kwmaba mchezo wa kesho inahitaji ushindi ili kujitoa kwenye nafasi hiyo na kupanda katika nafasi za juu, jukumu kubwa kwa mashabiki ni kuzidi kuwasapoti kwa namna yoyote pale inapokuwa uwanjani.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO JUMATANO MEI 11-2022
Next articleBRELA YATOA ELIIMU KWA WADAU NA WANANCHI KATIKA MAONESHO YA BIASHARA YA NCHI ZILIZO JILANI NA ZIWA TANGANYIKA KIGOMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here