Home LOCAL KIKOKOTOO KIPYA KUWAPA NEEMA WASTAAFU, WATAALAM WATOA ELIMU KWA WAHARIRI DODOMA

KIKOKOTOO KIPYA KUWAPA NEEMA WASTAAFU, WATAALAM WATOA ELIMU KWA WAHARIRI DODOMA

Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nyanda Shuli akitoa inayohusu Kanuni Mpya za Kikokotoo cha mafao ya Pensheni katika Kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya habari Mei 27,2022 Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania Deodatus Balile (kushoto) akizzungumza alipokuwa akiongoza zoezi la Wahariri kuuliza maswali kwenye kikao kazi hicho.
 

Mwanasheria wa NSSF Frank Mgeta (kushoto) akitoa ufafanuzi wa masuala ya Kisheria wakati wa Kikao kazi hicho kilichowakutanisha wahariri na Waandishi wa habari leo Mei 27,2022 Jijini Dodoma.

Festo Fute kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu akizungumza kwenye Kikao kazi hicho.
 

Mkurugenzi wa Adhari wa (PSSSF) Ansiger Mushi (kulia aliyesimama) Akizungumza kwenye Kikao kilichoandaliwa na OfisI ya Waziri Mkuu wahariri wa vyombo vya habari wakati wa kikao kazi hicho Jijini Dodoma.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi Gazeti la Nipashe na Mjumbe TEF Joseph Mwendapole akiuliza swali kwenye Kikao kazi hicho.


Kaimu Mkuu wa Chumba cha Habari Shirika la Utangazaji TBC 1 Anne Mwasyoke akiuliza swali,


Mhariri Mwandamizi na Mjumbe wa TEF kutoka UHURU Media aAngel Akilimali akiuliza swali kwenye kikao kazi hicho.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi na Mjumbe wa TEF Abdalla Majula akizungumza alipokuwa akiuliza maswali kwenye Kikao hicho.

Meneja Matekelezo wa PSSSF Victor Kikoti (katikati) Akizungumza alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa kikao kazi hicho Jijini Dodoma. (kulia) ni mwanasheria wa NSSF Frank Mgeta, na (wa pili kushoto) ni Lulu Mengele Meneja Mahusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF.Meneja Mahusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF Lulu Mengele akizungumza alipokuwa akifafanua jambo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika Kikao kazi hicho Mei 27,2022 Jijini Dodoma. 

Meneja Mahusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF Lulu Mengele akisisitiza jambo alipokuwa akjibu maswali ya Wahariri wa habari katika Kikao kazi hicho Jijini Dodoma. (kushoto), ni Meneja Matekelezo wa PSSSF Victor Kikoti, (kulia), ni Mhariri wa Gazeti la The East Africa Apolinary Tairo.

DODOMA.
SERIKALI imesema kuwa, kanuni mpya ya mafao ya pensheni inatarajia kuongeza
kiwango cha mkupuo wa mafao kutoka asilimia 25 iliyolalamikiwa mwaka 2018 hadi asilimia 33.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bw.Nyanda Shuli wakati akiwapitisha na kuwaelimishwa Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kuhusu kanuni mpya ya mafao ya pensheni 
inayotarajiwa kuanza Julai Mosi,2022.

Ni kupitia kikao kazi kati ya Wahariri na wataam mbalimbali kilichoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambacho kimefanyika Mei 27,2022 jijini Dodoma.

Bw.Shuli pia amesema,wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii watanufaika na ongezeko hilo kwani malipo ya mkupuo yatapanda kwa asilimia 81 ya wanachama na malipo ya pensheni yataongezeka kwa asilimia 19 ya wanachama.

“Kanuni inaongeza pensheni ya mwezi kutoka asilimia 50 ya sasa hadi asilimia 67 kwa wanachama wa PSPF na LAPF.

“Kanuni itaweka uwiano na usawa wa mafao baina ya wastaafu wote na itafanya mifuko kuwa imara na endelevu,”amesema Bw.Shuli.

Kamishna huyo amefafanua kuwa, kazi iliyofanyika kwa ushirikiano wa Wadau wa Utatu kwa maana ya Serikali,Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA)  na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) imewezesha kupata kanuni bora na endelevu.

Bw.Shuli amefafanua kuwa, Hifadhi ya Jamii inaimarisha ustawi wa jamii kwa kuweka mifumo inayowakinga wananchi dhidi ya majanga ya kijamii kama vile uzee, ulemavu, kifo, ugonjwa na kukosa ajira.

“Ipo mifumo ya uchangiaji au isiyo ya uchangiaji (misaada).Mifumo ya uchangiaji ina wanachama wanaochangia na hivyo kustahili huduma kulingana na sheria na kanuni zinazotumika.

“Mifumo ya uchangiaji inaipunguzia Serikali mzigo kupitia bajeti ya Serikali,”anafafanua Bw.Shuli.

Anaongeza kuwa,mifumo isiyo ya uchangiaji (misaada) ni kama vile TASAF na huduma za afya kwa wazee na makundi mengine.
 
WAHARIRI WA HABARI WAKIFUATILIA MKUTANO HUO.

Previous articleTAULO ZA KIKE 1000 ZAKABIDHIWA, VIJANA WAFUNDWA HEDHI SALAMA KINYAMWEZI SEKONDARI
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI ASUBUHI YA LEO JUMAMOSI MEI 28,2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here