Home LOCAL JIJI LA DAR ES SALAAM LAJIPANGA KUWA KINARA KWENYE ZOEZI LA SENSA...

JIJI LA DAR ES SALAAM LAJIPANGA KUWA KINARA KWENYE ZOEZI LA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022

 

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Tabu Shaibu akiwasilisha ajenda mbalimbali katika kikao kikao cha kawaida  cha robo ya tatu cha Baraza la madiwani ambacho kimefanyika leo katika ukumbi wa Anatorglo jiji  Dar es salaam.

Naibu Meya wa Jiji la Dar es salaam Saad Khimji akizungumza kwenye kikao cha kawaida  cha robo ya tatu cha Baraza la madiwani  ambacho kimefanyika leo katika ukumbi wa Anatorglo jiji

Baadhi ya wajumbe ambao wamehudhuria katika kikao kikao cha kawaida  cha robo ya tatu cha Baraza la madiwani ambacho kimefanyika leo katika ukumbi wa Anatorglo jiji  Dar es salaam.

NA: MUSSA KHALID.

Halmashauri  ya jiji la Dar es salaam imejipanga kufanikiwa kuwa kinara namba moja wa ufanikishaji zoezi la sensa ya watu na  makazi linalotarajiwa kufanyika nchini mwezi Agosti Mwaka huu.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na Naibu Meya wa jiji hilo Saad Khimji wakati akizungumza kwenye kikao cha kawaida  cha robo ya tatu cha Baraza la madiwani ambacho wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo ajenda ya maandalizi ya sensa mwaka huu.

Khimji ambaye amekuwa Mwenyekiti katika Kikao hicho amesema ili kufanikisha zoezi hilo wameunda kamati mbalimbali katika ngazi za Wilaya,Kata na Mitaa kuhakikisha wanasimamia usambazaji na matumizi ya matokeo ya sense baada ya kutangazwa rasmi.

‘Matarajio yetu ni kuona katika zoezi hili la sensa linalokuja basi tutafanya kiufanisi zaidi kiasi kwamba tunatarajia kushika namba moja kwa ufanikishaji wa zoezi kwa kushirikiana na viongozi wengine wa kiserikali ndani ya wilaya na Mkoa kwa ujumla hivyo kama Halmashauri ya jiji la Dar es salaam tupo tayari’amesema Naibu Meya Khimji

Aidha Naibu Meya huyo amesema zoezi la sensa lina manufaa na faida kubwa hivyo ametoa wito kwa wananchi wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha wanajipanga kwa ajili ya kuhesabiwa.

‘Katika utaratibu wa sensa madiwani wote wa Kata ni wenyeviti wa kamati za sensa katika Kata zao hivyo ni vyema wakaendelea kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Tabu Shaibu amesema maandalizi ya awali yameshaanza ili kufanikisha zoezi hilo la sensa na hivyo wamewataka madiwani kuendelea kuhamasisha wananchi kufahamu umuhimu wake.

Kuhusu zoezi la uombaji wa ajira za muda za Makarani na wasaidizi wa sensa ya watu na Makazi Bi.Tabu amesema limekamilika tangu mei 19 ambapo jumla ya maombi yaliyotumwa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam ni 22,562 kwa nafasi za Makarani,wasimamizi wa maudhui na wasimamizi wa TEHAMA na kati ya hayo maombi 19,539 yamekamilika na maombi 3,022 hayajakamilika.

Hata hivyo imeelezwa kuwa uelimishaji  na uhamasishaji wa sensa katika watu kushiriki  mwaka huu unaendelea kwa njia mbalimbali zikiwemo za mikutano kwa wananchi,vipeperushi pamoja na ujumbe mfupi kwa njia ya simu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here