NA: MWANDISHI WETU
SHINDANO la kumsaka mrembo atakaye wakilisha Tanzania, katika mchuano wa urembo dunia 2022 linatarajiwa kufanyika Mei 20 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Shindano hilo lilianza kufanyika mwaka jana kwa ngazi ya mikoa na kanda na kupata walimbwende 20 ambao wameingia kambini leo kwa ajili ya maandalizi ya kilele cha mashindano.
Akizungumza na ukurasa huu mmoja wa wadhamini wa mchuano huo Amina Swedi, amesema jukwaa hili ni mahususi kwa kuibua wasichana ambao wamekuwa chachu ya maendeleo katika taifa la Tanzania.
“Nikiwa kama mmiliki wa kampuni ya Itsallboutcards, iliyopo Mwenge, nimekubali kudhamini shindano hili kwa miaka minne mfululizo kwa sababu jukwaa la Miss Tanzania ni sehemu pekee inayompati msichana kuibua kibaji alicho nacho tumeshuhudia warembo wengi walioshiriki wakitumikia taifa katika nyanja tofauti serekalini hivyo nikiwa kama mwanamke mjasiria mali nitakuwa mstari wa mbele kufanikisha ndoto za mabinti hawa,” anasema Amina Swedi.
Shindano la Miss Tanzania mwaka huu lina andaliwa na kampuni ya The Look Campan Limited, ikiwa ni msimu wa nne kwa kampuni hiyo tokea kupata dhamana ya kuendesha michuano hiyo 2018.