Home BUSINESS CHONGOLO: WAMILIKI WA MIGODI SHINYANGA TOENI VIFAA VYA USALAMA KWA WACHIMBAJI WADOGO

CHONGOLO: WAMILIKI WA MIGODI SHINYANGA TOENI VIFAA VYA USALAMA KWA WACHIMBAJI WADOGO

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amewaelekeza viongozi wa Serikali wilayani Shinyanga kusimamia wamiliki wa migodi ili watoe zana za usalama kwa wachimbaji wadogo wa madini.

Katika maelekezo yake, Chongolo amesema zana za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo ni wajibu wa wamiliki wa migodi wanaowafanyia kazi.

Ametaka wamiliki hao kutoa zana hizo kwa wachimbaji wadogo ili kuwaepushia madhara wakati wa shughuli hizo.

Ili kufanikisha hilo, ameielekeza Serikali wilayani Shinyanga kusimamia utekelezaji wa hilo.

“Simamieni wale wachimbaji wadogo kwenye haya maeneo kupewa zana za uchimbaji, ili watendewe haki. Sio busara mtu anakwenda mahali anachimba anapata anaondoka wanaomchimbia anawaacha wakiwa na madhara yaliyotokana na kutotumia zana nzuri,” amesema.

Awali, baada ya kukagua mradi wa tenki la maji katika Kata ya Mwakitolyo, Chongolo amewataka wananchi kuitunza miundombinu ya maji inayojengwa na Serikali.

“Najua wananchi wengi wa eneo hili ni wachimbaji, wakati wa shughuli zenu mtakapokuta mabomba msiyakatekate, kufanya hivyo kutakwamisha hata shughuli zenu,” amesema.

Pia, ameiagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (RUWASA), kuharakisha usambazaji wa mabomba na kufikisha maji kwa wananchi baada ya mradi kukamilika.

Kwa mujibu wa Chongolo, mradi wa tenki hilo lenye ukubwa wa lita 500,000 na unatarajiwa kuhudumia wananchi 16,400 umetekelezwa kwa Sh394.1 bilioni zinazotolewa na Serikali na kwamba mradi upo asilimia 98.

Previous articleKONGAMANO LA AIESEC LAFANYIKA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI (MoCU)
Next articleSHAKA AONGOZA MAPOKEZI YA MEMBE KWA KISHINDO NA KUMKABIDHI KADI YA UANACHAMA WA CCM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here