Home BUSINESS BENKI YA CRDB KUENDELEA KUTOA MIKOPO YA WAFANYAKAZI KWA RIBA YA CHINI

BENKI YA CRDB KUENDELEA KUTOA MIKOPO YA WAFANYAKAZI KWA RIBA YA CHINI


Wakati Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ikiboresha maslahi ya wafanyakazi nchini pia kushusha tozo mbalimbali katika mishahara, Benki ya CRDB imepandisha kiasi cha mkopo wanachoweza kuchukua wafanyakazi pia kuongeza muda wa marejesho hadi kufikia miaka saba ili kufanikisha shughuli zao za kiuchumi.

Kwenye maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema, benki itaendelea kutoa mikopo kwa wafanyakazi (personal loan) kwa riba ya chini ili kuwaongezea kiasi wanachoweza kukopa. Alisema benki imeshusha riba hiyo kutoka 16% hadi 12% hivyo kuongeza kiwango cha kukopa hadi Sh200 milioni kitakachorejeshwa mpaka kwa miaka saba.

 
“Maboresho haya ni sehemu ya mkakati wa Benki ya CRDB kusaidia jitihada za Serikali kuboresha maisha ya wafanyakazi nchini,” amesema Nsekela.

Maboresho mengine Nsekela amesema yamefanyika kwenye Salary Account ambayo ni akaunti maalaum kwa ajili ya wafanyakazi inawawezesha kupokea mshahara kwa urahisi. Akaunti hii imeunganishwa na huduma za kidijitali za SimBanking na Internet banking ili kumwezesha mfanyakazi kupata taarifa na kufanya miamala kwa urahisi kutoka mahali popote alipo ndani hata nje ya nchi.


“Huduma hizi zimekuwa mkombozi mkubwa kwa wafanyakazi hususani waliopo maeneo ambako hakuna matawi yetu kwani husaidia kupata huduma zote kiganjani ikiwamo huduma ya mkopo wa kidijitali wa Salary Advance ambao hivi karibuni kiwango cha kukopa kiliongezwa hadi Sh3 milioni,” amefafanua Nsekela.
 
 

Kwa kushirikiana na Taasisi za Serikali, Nsekela amesema Benki ya CRDB imejipanga vyema kuhakikisha mipango ya wafanyakazi inakamilishwa kwa wakati kupitia mtandao wake mpana wa huduma.

Amesema Benki ya CRDB inaongoza katika hilo kwani inao mtandao mpana wa kutolea huduma ikiwa na matawi 268 na mawakala (CRDB Wakala) zaidi ya 20,000 waliosambaa kila kona ya nchi, kuanzia mjini mpaka vijijini hivyo kuwawezesha wafanyakazi kupata huduma katika maeneo yao ya kazi hali inayowasiaidia kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za benki.
 


Kwa wateja wanaopata matatizo ya kifamilia, Nsekela amesema Benki ya CRDB inayo Kava Assurance, huduma ya bima ya maisha ambayo imeunganishwa na akaunti ya mteja inayomwezesha kupata mkono wa pole kuanzia Sh2 milioni hadi Sh15 milioni pindi mwenza wake anapofariki au kuwafariji warithi wake yeye mwenyewe akifariki.

Benki ya CRDB kwakushirikiana na Serikali ya mkoa wa Dodoma chini ya Mkuu wa Mkoa ilifanikisha sherehe hizo kwa kuwa mzamini mkuu ikitekeleza kauli mbiu yake ya Tupo Tayari, kufanya kazi Bega kwa Bega na Serikali katika kufanikisha maendeleo ya Taifa letu.
 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akifurahi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela mara baada ya kumalizika kwa sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri-Dodoma.

Tawi linalo tembea(Mobile Branch) likipita mbele ya Mgeni Rasmi katika kusindikiza maadamano ya wafanyakazi.
Previous articleSHIRIKA LA SMCCT LAKUWATANISHA WADAU KUCHANGIA SH.MILIONI 5 KUSAIDIA WANAWAKE NA WASICHANA MKOANI SINGIDA
Next articleWAZIRI DKT. GWAJIMA ATOA MREJESHO MIKUTANO YA KIMATAIFA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here