Home SPORTS YANGA, SIMBA HAKUNA MBABE

YANGA, SIMBA HAKUNA MBABE

Na: mwandishi wetu.

MABINGWA watetezi, Simba SC wametoa sare ya bila mabao na vinara wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Benjamin.

Hata hivyo katika mchezo huo leo  Inonga alimdhibti vyema Mayele, kinara wa mabao Ligi Kuu ambaye muda wote wa mchezo alipiga shuti moja tu lililogonga nyavu za pembeni, nje kulia kipindi cha pili.

Simba pekee waliofanya jaribio la hatari lililolenga lango, Mkongo mwingine, mshambuliaji Chris Kope Mutshimba Mugalu alipounganishia mikononi mwa kipa Djigui Diarra mpira wa adhabu wa beki Shomari Kapombe kipindi cha pili pia.

Hata hivyo mchezo wa leo ulikuwa WA ushindani na kukamiana na kuonyeshana ubabe baina ya wachezaji wa pande zote mbili na pongezi kwa refa chipukizi, Ramadhani Kayoko kwa kuimudu pamoja na makosa machache ya kibinadam aliyoyafanya.

Kwa sare hiyo, Simba wanafikisha pointi 42 baada ya mechi 20, wakizidiwa pointi 13 na watani wao wa jadi, Yanga ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi.

Watani hao wa jadi wanaweza kukutana tena kabla msimu kufungwa katika mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), iwapo Simba wataitoa Pamba FC ya Mwanza.

Previous articleWWF YAZINDUA MPANGO WA ELIMU YA UHIFADHI NA MAZINGIRA KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Next articleMHE. KIGAHE AZINDUA JENGO LA UTAWALA LA KIWANDA CHA MATI SUPER BRAND LTD NA BIDHAA YA TANZANITE PREMIUM VODKA BABATI MKOANI MANYARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here