Home LOCAL WIZARA YA AFYA YAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA KIKAO KAZI JIJINI...

WIZARA YA AFYA YAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA KIKAO KAZI JIJINI DAR

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Afya, Bi. Catherine Sungura akizungumza wakati wa kikao kazi kati ya Wizara na waandishi wa habari kujadiliana na kushauriana masuala ya habari ili jamii izidi kupata taarifa zaidi kuhusu afya.

Mkurugenzi wa FullShangwe Blog, John Bukuku, akichangia jambo wakati wa kikao kazi kati ya Wizara ya Afya na waandishi wa habari, kilichoandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.

Mwandishi wa masuala ya afya na jamii wa Matukio na Maisha Blog, Veronica Mrema akiwasilisha maoni yaliyotolewa na kundi A, wakati wa kikao kazi kati ya Wizara ya Afya na waandishi wa habari, kilichosimamiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo, Catherine Sungura, lengo ikiwa kujadiliana na kushauriana wapi Kitengo hicho kifanye maboresho ili jamii izidi kupata taarifa zaidi kuhusu afya.


Mwandishi wa ITV, Richard Stephani akiwasilisha maoni yaliyotolewa na kundi B, wakati wa kikao kazi kati ya Wizara ya Afya na waandishi wa habari, kilichosimamiwa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara hiyo, Catherine Sungura, lengo ikiwa kujadiliana na kushauriana wapi Kitengo hicho kifanye maboresho ili jamii izidi kupata taarifa zaidi kuhusu afya.


Mwenyekiti wa waandishi wa habari waliohudhuria kikao kazi hicho Vincent Kasambala kutoka Upendo Media akizungumza jambo katika kikao kazi hicho kilichowakutanisha waandishi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam.

  Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, wakiwa katika kikao kazi kati ya Wizara ya Afya na waandishi wa habari, katika kikao hicho waandishi wa habari walijengewa uelewa kuhusu mikakati na vipaumbele vya Wizara ya Afya katika kuwahudumia wananchi.Kikao hicho kiliandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini -Wizara ya Afya

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here