Home LOCAL WAZIRI BASHUNGWA ATOA MAAGIZO KWA MAKATIBU TAWALA KUHUSU VIFAA VYA TEHAMA

WAZIRI BASHUNGWA ATOA MAAGIZO KWA MAKATIBU TAWALA KUHUSU VIFAA VYA TEHAMA

  

Na. Angela Msimbira Dar Es Salaam

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa kuhakikisha vifaa vinafika katika vituo kwa kuzingatia mgao uliotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI

Ametoa agizo hilo leo tarehe 25 Aprili, 2022 wakati wa kuzindua usambazaji wa vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya Vituo vya Walimu (Teachers’ Resource Centres- TRCs) 150 vilivyopo katika Halmashauri 144 za Mikoa 26 ya Tanzania Bara luliofanyika Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa, Jijini Dar-es-salaam.

Waziri Bashungwa amewaagiza ,Makaatibu Tawala wa Mikoa kuhakikisha wanawasilisha taarifa ya mapokezi na usambazaji wa vifaa hivyo kimkoa kwa Katibu Mkuu – Ofisi ya Rais – TAMISEMI kabla au ifikapo tarehe 15 Mei, 2022;

Amewataka Makatibu hao kuhakikisha wanasimamia ufundishaji na ujifunzaji ili matokeo ya Mitihani ya Taifa na Ubora wa Elimu viendane na kiwango kikubwa cha uwekezaji unayofanywa na Serikali..

Amesema kuwa Serikali imeamua kuvifufua vituo hivyo kwa lengo kusaidia walimu kubadilishana uzoefu, hali kadhalika wataalam wabobezi kupeana mbinu za ufundishaji wakiwa na walimu, ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu ya msingi na sekondari nchini.

Ameendelea kufafanua kuwa hadi sasa tayari Halmashauri 144 zimeanza kutekeleza Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA). Walimu 12,544 tayari wameshapatiwa mafunzo, na lengo ni kuwafikia walimu 30,957 katika mwaka huu wa fedha.

Waziri Bashugwa ameziagiza Halmashauri zote nchini katika mwaka wa fedha 2022/2023 kuhakikisha wanatenga bajeti ya maeneo ya kujenga vituo hivyo vya TEHAMA ili Halmashauri zote nchini zoweze kuwa na vituo hivyo muhimu katika kipindihiki chenye mabadiliko makubwa ya Sayansi na Teknolojia
Aidha vifaa vilivyogawiwa ni mashine ya kudurufu 150, printa 150 projekta 150 na kompyuta za mezani (desktop computers) 600 vilivyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.5

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here