Home LOCAL WATU 23 WAKATWA MAPANGA CHANIKA

WATU 23 WAKATWA MAPANGA CHANIKA

HERI SHAABAN

WANANCHI 23 Wakazi wa Zingiziwa  wanadaiwa KUKATWA mapanga usiku wa Leo na Kundi la Vibaka wamepokelewa kupatiwa matibabu Katika hospitali ya Nguvu kazi CHANIKA wanaendelea vizuri .

Akizungumza Waandishi wa habari leo asubuhi nyakati tofauti Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dkt. Eldhabeth Nyema, alisema ni kweli Alfajili ya Leo amepokea Wananchi walioshambuliwa kwa Mapanga na visu na watu wasiofamika

“Katika hospitali yetu Chanika Nguvu Kazi Wilaya ya Ilala Alfajili ya Leo tumepokea  wagonjwa 23 na wanne wameamishiwa Hospitali ya Rufaa Mkoa AMANA  na wagonjwa 19 walikuwa wanaendelea kuhudumiwa na kuruhusiwa wengi wameshonwa sana Nyuzi alisema Dkt Eldhabeth.

MGANGA Mkuu Dkt, Eldhabeth alisema taarifa kuhusu hali za wagonjwa ataendelea kutupa taarifa katika tukio hili kubwa ambalo limewakumba wakazi wa eneo hilo

DIWANI wa Kata ya Zingiziwa MAIGE MAGANGA alisema tukio hilo ambalo limeikumba Kata yake ya Zingiziwa analaani vikali ambalo limefanywa na Vijana wanaodaiwa PANYA ROAD usiku wa Leo Mtaa wa GOGO waliotumia mapanga ,silaha za jadi na marungu.

DIWANI MAIGE MAGANGA alisema tukio hilo ambalo limeikumba Kata yake Zingiziwa alivumiliki awezi kuacha Jamii idhidi kuharibikiwa kwa vijana wanaoishi Eneo hilo.

Diwani Maige ametoa agizo kwa Wananchi wake wa Zingiziwa kutoa taarifa katika vyombo vya ulinzi na Usalama ngazi ya Kata,Mtaa na Wilaya Ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua

Diwani Maige ametoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija kwa kuchukua hatua haraka Kukabiliana na Janga hilo la Wananchi kuvamiwa ambapo walifika katika hospitali ya CHANIKA nguvu kazi na kupatiwa matibabu haraka.

“Natoa shukrani kwa dhati  Hospitali ya Nguvu Kazi kuweza kuwapokea na kuwahudumia kwa haraka Waanga wa tatizo hili /Uvamiaji na wameweza kuwahudumia majeruhi wote, Shukrani kwa Mh.Mbunge Jerry Slaa kwa ushirikiano wake wa haraka kupata Huduma hizi kwa Haraka,na Shukrani kwa MGANGA Mkuu wa  Wilaya ya Ilala, pamoja na  ZCO ameweza pia kufika eneo hili kwa dharura na haraka, na Shukrani za mwisho wananchi wote tulioweza kushirikiana kuhudumia majeruhi Hawa na kuwafikisha Hospitali”Diwani Maige Maganga.

Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija alisema anatarajia kufanya ziara Leo mchana eneo hilo kuangalia Usalama wa Wananchi na kuimalisha Ulinzi.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija amewataka Wananchi kuwa watulivu kwa Sasa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ilala wanafatilia tukio hilo

Hata hivyo tulipowasiliana na Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam Jumanne Mulilo simu yake ya mkononi ilikuwa aipatikani .

Mwisho.

Previous articleWAFUGAJI IGUNGA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA MRADI
Next articleMATUKIO KATIKA PICHA WASHINGTON DC
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here