Home LOCAL WANANCHI WAISHUKURU RUWASA KISHAPU KUWAFUNGIA MOTA MPYA MRADI WA MAJI NG’WANG’HOLO –...

WANANCHI WAISHUKURU RUWASA KISHAPU KUWAFUNGIA MOTA MPYA MRADI WA MAJI NG’WANG’HOLO – NYENZE

Mhandisi kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu, Nicholaus Mathias (wa pili) kushoto na Mhandisi kutoka Kampuni ya Ukandarasi Hydrotech, Innocent Msacky ( wa kwanza kushoto) wakiwa wameshikilia Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo. Katikati ni Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima, wa kwanza kulia ni Katibu wa Kamati ya Watumiaji Maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo, Anna Moshi.

Na: Kadama Malunde – Malunde 1 blog.
Wananchi wa vijiji vya Ng’wang’holo na Nyenze kata ya Mwadui – Lohumbo wilayani Kishapu wameishukuru Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga kwa kuwafungia Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo na Kiimarishaji ‘Stabilizer’ kutokana na iliyokuwepo kuharibika kutokana na hitilafu ya umeme.

RUWASA Kishapu imetumia shilingi Milioni 5 kwa ajili ya kununua na kufunga Mota ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji na Kiimarishaji ‘Stablizer’ katika mradi huo wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.

Wakizungumza leo Jumatano Aprili 20,2021 wakati wakishiriki zoezi la kufunga mota hiyo pamoja na Stablizer vilivyonunuliwa na RUWASA Kishapu, wananchi wamesema sasa wataanza kupata huduma ya maji safi na salama baada ya mota kuharibika mwezi Desemba 2021.

Mmoja wa wakazi wa Ng’wang’oholo Bi. Sayi Kulwa amesema baada ya mota hiyo kuharibika wamekuwa wakitumia muda mrefu kutafuta huduma ya maji kwenye mabwawa na mito.

“Maji yamekuwa ya shida sana hali iliyokuwa inatulazimu kuamka usiku kufuata maji kwenye visima vilivyochimbwa pembezoni mwa mito. Maji hayo siyo salama lakini pia tunahatarisha maisha yetu kwa kushambuliwa na wanyama wakali lakini watoto wa kike wanaweza kubakwa sambamba na ndoa kuvunjika. Tunawashukuru RUWASA kwa kusikia kilio chetu na sasa tumefungiwa mtambo huu tuanze kupata huduma ya maji safi na salama”,amesema Kulwa.

“Tunashukuru RUWASA kwa kutupatia mtambo huu, baada ya mota kuharibika tulianza tena kufuata maji kwenye mabwawa na mito,maji ambayo kimsingi hayakuwa salama, lakini sasa tutapata maji safi na salama”,ameongeza Tungu Kwangulija.

Naye Bw. Sumai Salum Sabhi amesema licha kwamba mradi huo unanufaisha vitongoji viwili vya Ng’wang’holo na Nyenze, kufungwa kwa mtambo huo kutaondoa changamoto ya wananchi hasa akina mama kutumia muda mrefu kutafuta maji hivyo kushiriki katika shughuli za maendeleo huku akiomba serikali kuwapatia huduma ya maji ya Ziwa Victoria kutokana na kwamba bomba la maji hayo linapita kwenye eneo lao kuelekea wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Ng’wang’holo Bw. William Bulugu Kabisi mradi wa maji Nyenze – Ng’wang’holo uliojengwa na RUWASA Kishapu, umesaidia kupunguza shida ya maji katika vitongoji viwili vya kijiji cha Ng’wang’holo na Nyenze.

“Tunawashukuru RUWASA kwa kusikiliza na kufanyia kazi ombi letu tulilolitoa kupitia Kamati ya watumiaji maji kwenye mradi huu kuwa tunahitaji kupatiwa Mota mpya baada ya ile iliyokuwepo kupata hitilafu. Leo wametufungia mtambo/kifaa hiki ili kutatua changamoto ya maji kwa wananchi ambao wamekuwa wakilazimika kutumia maji yasiyo salama kutoka kwenye Chemchemi, mito na mabwawa”,amesema Kabisi.

Mwenyekiti huyo wa kijiji ametumia fursa hiyo kuiomba serikali kuwapatia huduma ya maji kwenye vitongoji vilivyosalia ili wananchi wote katika vijiji vya Nyenze na Ng’wang’holo wapate huduma ya maji safi na salama.

Katibu wa Kamati ya Watumiaji Maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo, Anna Moshi amesema sasa huduma ya maji safi na salama itapatikana baada ya mota mpya kufungwa tangu iharibike mnamo Desemba 27,2021 huku akibainisha kuwa bei ya maji kwa ujazo wa lita 20 ni shilingi 50 na Unit moja ni shilingi 2500.

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima amesema mradi wa maji ya kisima kirefu cha Ng’wang’holo – Nyenze ulikamilika mwaka 2020 baada ya RUWASA kufanya maboresho ya mradi kutoka Kisima cha mkono ‘Pampu ya mkono’ na sasa una vituo sita vya kuchotea maji ukihudumia wananchi zaidi ya 3000.

Tulifanya maboresho ya mradi huu kupitia fedha za Programu ya Lipa kwa Matokeo (PBR) shilingi Milioni 72. Baada ya kumaliza kuboresha mradi huu wananchi walianza kupata huduma ya maji safi na salama lakini tarehe 27,2021 Desemba 2021 mota iliungua kutokana na hitilafu ya umeme”,amesema Mhandisi Kamazima.

“Baada Mota ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji kuharibika, Kamati ya watumiaji maji iliandika barua ikaomba RUWASA inunue kifaa kilichoharibika. RUWASA huwa tuna fungu la uendelevu wa miradi ya maji hivyo tulipokea ombi hilo lakini tulikwama kutokana na taratibu za manunuzi lakini leo tunafunga mota mpya na Stabilizer kupitia Mkandarasi Hydrotech ili wananchi waanze kupata huduma ya maji mara moja kama hapo awali”,amesema Mhandisi Kamazima.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI

Mhandisi kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu, Nicholaus Mathias (wa pili) kushoto na Mhandisi kutoka Kampuni ya Ukandarasi Hydrotech,  Innocent Msacky ( wa kwanza kushoto) wakiwa wameshikilia Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo. Katikati ni Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima, wa kwanza kulia ni Katibu wa Kamati ya Watumiaji Maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo, Anna Moshi. Kifaa kingine chini ni Kiimarishaji ‘Stablizer’ . Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog/.
 

Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima (kushoto) akiangalia Kiimarishaji ‘Stablizer’ katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo kata ya Mwadui – Lohumbo wilayani Kishapu.

 

Wananchi wakiwa kwenye eneo la mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo kata ya Mwadui – Lohumbo wilayani Kishapu.

Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima  akionesha Tanki la maji kwenye mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo kata ya Mwadui – Lohumbo wilayani Kishapu.
 

Mhandisi kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu, Nicholaus Mathias (kulia) na Mhandisi kutoka Kampuni ya Ukandarasi Hydrotech,  Innocent Msacky wakirekebisha mfumo wa umeme katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo kata ya Mwadui – Lohumbo wilayani Kishapu.
 

Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima akizungumza wakati wa zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo. Kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha Ng’wang’holo Bw. William Bulugu Kabisi.
 

Mhandisi kutoka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu, Nicholaus Mathias (kushoto) na Mhandisi kutoka Kampuni ya Ukandarasi Hydrotech,  Innocent Msacky wakifunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
 
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima (kulia) akizungumza wakati wa zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
 

Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima (kulia) akishirikiana na wananchi kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
 

Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Protas Kamazima (kulia) akishirikiana na wananchi kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
 

Wananchi wakishiriki zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
 

Wananchi wakishiriki zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.

Wananchi wakishiriki zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
 

Wananchi wakishiriki zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo.
 

Zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo likiendelea.
 

Zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo likiendelea.
 
Zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo likiendelea.
 

Mwenyekiti wa kijiji cha Ng’wang’holo Bw. William Bulugu Kabisi akiishukuru RUWASA Kishapu Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo wilayani Kishapu.
 

Katibu wa Kamati ya Watumiaji Maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo, Anna Moshi akielezea namna wananchi watavyonufaika na mradi wa maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo wilayani Kishapu.
 
Akina mama wakizungumza wakati wa zoezi la kufunga Mota mpya ya kuendesha Pampu ya kusukuma maji katika mradi wa maji safi wa Nyenze – Ng’wang’holo wilayani Kishapu.

Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here