Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (Katikati) akiwa na viongozi wa kamati ya amani
Na: Hellen Mtereko, Mwanza
Viongozi wa kamati ya amani Mkoani Mwanza wamepewa elimu ya anwani za makazi ili waweze kwenda kuwaelimisha waumini wao hali itakayosaidia jamii kutambua,kufahamu umuhimu wa kuwa na anwani.
Elimu hiyo imetolewa leo hii Aprili 7,2025 kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabliel, amesema kuwa viongozi wa dini wanamakundi makubwa ya watu hivyo kupitia elimu hii ninaimani mtakwenda kuwa walimu wazuri wakuwafundisha waumini wenu
Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu inadhamira ya kuwasaidia Wananchi katika kuboresha mwasiliano kwenye sehemu mbalimbali ikiwemo makazi yao,sehemu zao za biashara, na maeneo mengine ya huduma za kijamii.
Abdul Mzee ni mratibu wa anwani za makazi Mkoa wa Mwanza amesema wameamua kutoa elimu kwa kamati ya amani ya Mkoa inayo husisha viongozi wa dini kutoka madhehebu ya Kikristo na waisilam kwa sababu wanaamini elimu ikifika kwa viongozi hao itafika kwa kila mwananchi.
Amesema kuwa kwa kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani,kwaresima misikitini na makanisani waumini wanakuwa wengi hivyo viongozi wa dini wakitumia muda huu elimu itawafikia wengi.
Mzee amesema kuwa kwa Mkoa wa mwanza nyumba 653,827 zimewekewa namba sawa na asilimia 118.54 ya lengo ambapo hadi sasa nyumba 421,212 zimesajiliwa kwenye mfumo sawa na asilimia 64.42.
Ameongeza kuwa wanatarajia kumaliza zoezi hilo ndani ya siku saba kwani hadi sasa nguzo 6,007 zinazoonyesha majina ya barabara zimewekwa sawa na asilimia 25 ya lengo
Aidha amesema kuwa Mkoa unaendelea kutoa elimu ya anwani za makazi kwa makundi mbalimbali
Shekh wa Mkoa wa Mwanza Hasan Kabeke ambae ni Mwenyekiti mwenza wa kamati ya amani amesema kuwa mafunzo hayo yamemuwezesha kufahamu namna majina ya mitaa na namba zinavyopatikana kupitia simu ya mkononi
Pia amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maafisa wa anwani za makazi wapokuwa wanapita ili kuweza kusaidia zoezi hilo kwenda kwa wakati.
Nae mjumbe wa kamati ya amani Mkoa wa Mwanza Askofu Lameck NKumba, amesema kuwa kutokana na elimu iliyotolewa ya utambuzi wa anwani za makazi naamini kwa upande wa Taasisi za kidini itatusaidia sana kwani tutajulikana kuanzia jina la kanisa,wapi lilipo.
Credit – Fullshangwe Blog.