Home LOCAL TANZANIA NA INDIA KUIMARISHA UTOAJI WA HUDUMA ZA TIBA

TANZANIA NA INDIA KUIMARISHA UTOAJI WA HUDUMA ZA TIBA

Na:WAF-Dodoma.

Tanzania na India zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika utoaji wa huduma za tiba baina ya nchi hizo mbili kupitia Hospitali ya Apolo yenye makao makuu nchini India.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi  wakati wa kikao na Makamu wa Rais anayeshughulika na Ukuaji wa Biashara wa Hospitali ya Apollo, Bw Radhey Mohan.

Prof. Makubi amesema kuwa katika mazungumzo yao wamekubaliana kukuza ushirikiano uliopo katika masuala ya kubadilishana uzoefu katika utoaji wa huduma za tiba. 

Aidha, Prof. Makubi amemshukuru Bw. Mohan kwa kuwapatia matibabu bora Watanzania wanaopewa Rufaa ya kutibiwa katika Hospitali za Apollo zilizopo nchini India. Aidha Serikali inaendelea kuimarisha huduma za kibingwa ili watalaamu waweze kuzitoa hapa hapa nchini . 

“Tunawashukuru kwa kuwezesha utoaji wa mafunzo ya huduma kibingwa na ubingwa bobezi kwa wataalam kutoka Hospitali za Taifa pamoja na matibabu kwa watanzania tunaowapa rufaa kuja kutibiwa kwenye hospitali yenu”.

Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Hospitali ya Apollo Bw. Mohan aliishukuru Wizara ya Afya kwa kuendelea kuiamini Hospitali hiyo na kupeleka wagonjwa wanaohitaji matibabu ambayo hayapatikani hapa nchini. 

Bw.Mohan ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali wakati wowote unapohitajika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here