Home Uncategorized REKEBISHENI MAPUNGUFU YALIYOPO SHIMMUTA

REKEBISHENI MAPUNGUFU YALIYOPO SHIMMUTA

Na: Stella Kessy, DAR.
Afisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Allen Alex amewataka viongozi wapya wa Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma,Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA) kurekebisha mapungufu yote yaliopo, kwa maendeleo ya Shirikisho pamoja na michezo nchini.

Hayo ameyasema leo tarehe 9 Aprili, 2022 baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho hilo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) Jijini Dodoma.

“Kwanza kabisa nawapongeza kwa kuaminiwa na wajumbe kuweza kuwachagua kama viongozi wao, sasa mnapaswa kuwatumikia kwa juhudi zote, lakini pia mmeona kuna baadhi ya mapungufu yaliopo katika sehemu chache kwenye Shirikisho lenu, kwa mfano bado katiba yenu mnahitaji kuendelea kuiboresha ndani ya muda mfupi, ili kuendana na kasi mnayohitaji” amesema Allen.

Kwa upande wake rais mpya wa SHIMMUTA, Roselyne Massam amewahakikishia wajumbe  waliomwamini na kumchagua, kuwa atashirikiana na watu wote ili kutimiza malengo yaliyowekwa na maagizo yaliyotolewa na uongozi wa BMT.
Previous articleBENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI RUANGWA
Next articlePOLISI WAISHIKA PABAYA SIMBA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here