Na: Mwamvua Mwinyi, Kibaha,April 20
MKUU wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge amekemea baadhi wafanyabiashara wa Chakula Mkoani humo ,kuacha kugeuza mwezi huu wa kuvuna Faida kwa kuongeza Bei ya vyakula kiholela.
Akizindua msikiti wa Masjid E Mariya na kutoa misaada ya vyakula kwa Ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani vilivyotolewa na Taasisi ya kiislam ya Miraaj Tanzania ,huko Visiga Kwa Kipofu,Kibaha aliwataka kuacha kuongeza Bei za vyakula ukizingatia Ni mwezi wa Toba Jambo ambalo sio jema na linasababisha manung’uniko ndani ya jamii.
“Mwezi huu ni wa ibada wa Toba, wasiugeuze Ni mwezi wa kuvuna pesa ,Bali watoe Bei nzuri na iliyoelekezi bila kuongeza gharama mnakuwa hamtendi wema na mnaenda nje ya maadili ya upendo na ushirikiano kwani unasababisha manunguniko”
Vilevile, mkuu huyo wa mkoa aliiasa, jamii kuzingatia elimu kwani ndio urithi kwa watoto wetu kwa maisha yao baadae.
“Tufanye ibada kwa wingi ,Lakini watoto wapewe elimu ya dini kwa maslahi yao baadae ,na kuwapa maadili mema ya kidini .”
Alimshukuru aliyetoa eneo la msikiti Allah atamlipa kulingana na alichokitoa kwa Ajili ya kujengwa nyumba ya ibada.
Allah atupe Imani,wengi Wana Mali Lakini unakuta zinatumika vibaya ,nimefarijika kuona wewe umefanya Jambo jema la kutoa Mali kwa nia ya kufanya ibada”Nitasaidia kupimwa eneo hili ili kuondoa migogoro huko baadae “alisema Kunenge.
Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya Miraaj Tanzania, Arif Surya alisema Taasisi Yao imeungana na Taasisi mbalimbali za nje ikiwemo Eden Foundation kutoa msaada wa vyakula kwa watu 102 na kujenga msikiti huo.
Arif ametoa wito kutoa swadaka Kama hizo na ameomba Taasisi za aina hiyo ziungane kusaidia jamia.
Sheikh mkuu mkoa wa Pwani,Hamis Mtupa alihimiza amani kuhakikisha amani inapatikana kuanzia ngazi ya chini kuanzia Vijijini.
.
“Tuzingatie watu wanaotia wasiwasi tusiwakaribishe katika maeneo yetu”alisisitiza Mtupa.
Mtupa aliwashukuru Taasisi ya Miraaj Tanzania kwa kutoa msaada wa vyakula kwa Ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,na kusaidia ujenzi wa msikitil.