Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa maafisa Ugani wa Kilimo katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa pikipiki 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani Kilimo wa nchi nzima katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akimkabidhi mfano wa Ufunguo wa Pikipiki Waziri wa Kilimo Hussein Bashe mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani Nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu akiwasha Pikipiki mara baada ya kuzindua ugawaji wa pikipiki hizo 7000 kwa ajili ya Maafisa Ugani nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akumuelezea kuhusu bidhaa mbalimbali za Kilimo kabla ya kuzindua na kugawa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wa Kilimo nchini katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo la Taifa Jacqueline Mkindi kuhusu zao jipya la kilimo pamoja na mazao mbalimbali ya Biashara katika Maonesho yaliyofanyika nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiangalia miche ya matunda ya miembe pamoja na michungwa katika mabanda ya Maonesho ya bidhaa za kilimo nje ya ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma leo tarehe 04 Aprili, 2022.