Home BUSINESS NMB NMB YASHIRIKI KATIKA HAFLA YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI KATIKA...

NMB NMB YASHIRIKI KATIKA HAFLA YA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI KATIKA AWAMU YA TATU YA UJENZI WA RELI KUTOKA MAKUTUPORA MPAKA TABORA.


Afisa Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya NMB – Emmanuel Akonaay akimuelezea Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa, jinsi benki ya NMB ilivyoshiriki katika mradi wa SGR kupitia wakandarasi wa mradi huo kwanzia Dar- Morogoro, Morogora- Dodoma mpaka sasa, Makutupora- Tabora. Pia, namna benki ilivyowawezesha wazabuni wa mradi huo kwa kuwapa mitaji na kuhakikisha watumishi wanalipwa kupitia Benki ya NMB.


Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Sospeter Magesse(kulia), akizungumza na wajasiliamali ambao ni wateja wa NMB waliofika katika viwanja vya Cheyo B, Tabora kwa ajili ya kuuza na kuonesha bidhaa zao ambao pia wengi ni wazabuni katika mradi wa SGR.

Wateja wa NMB wakipata huduma mbalimbali katika banda la benki hiyo katika viwanja vya Cheyo B.

Kama ilivyokuwa katika miradi mbalimbali ya kimkakati, Benki ya NMB imeendelea kuwa mstari wa mbele kwenye kutoa ushirikiano kwa Serikali na Wakandarasi ili kuhakikisha miradi inayojengwa kwa manufaa ya Watanzania inakamilika kwa wakati.

Katika mradi wa reli ya kisasa ya SGR, Benki ya NMB imeshiriki katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika awamu ya tatu ya ujenzi wa reli hiyo yenye urefu wa kilomita 368 kutoka Makutupora mpaka Tabora. Mbali na kuwa wabia katika mradi huu mkubwa, benki hiyo imedhamini shughuli hii ya uwekaji wa jiwe la msingi iliofanyika katika viwanja vya Cheyo B, Tabora.

Previous articleSERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA CDC KUDHIBITI MAGONJWA
Next articleRUVUMA YAUPIGA MWINGI UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI KUPITIA FEDHA ZA UVIKO – 19
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here