Home BUSINESS NIC YATARAJIA KUTOA GAWIO KWA SERIKALI

NIC YATARAJIA KUTOA GAWIO KWA SERIKALI


Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam. 
 
 
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NIC, Bw. Laston Msongole akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elirehema Doriye akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za NIC Jijini Dar es Salaam.

NA: EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika la Bima la Taifa NIC linatarajia kutoa Gawio kwa Serikali baada ya kufanya vyema kwa kuongeza mitaji na shirika kujijengea uwezo mkubwa wa kujisimamia ambapo gawio wanalotarajia kutoa ni shilingi bilioni 1.5 na bilioni 12 .05 kuwekwa kama mtaji.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 20,2022 Jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NIC, Bw. Laston Msongole amesema kwa kipindi cha miaka minne mfululizo iliyopita kwa hesabu zilizokaguliwa inayonyesha kufanya vizuri baada ya taarifa ya hesabu ya mkaguzi mkuu wa Serikali CAG ,ambapo shirika limeendelea kuongeza faida.

“Miaka minne mfululizo iliyopita kufikia mppaka Juni, 2021 ambapo tunahesabu zilizokaguliwa, Shirika limekuwa na maendeleo yakutosha na hilo linathibitishwa na taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali ambaye huwa kila mwaka anakagua”. Amesema

Amesema katika kipindi cha mwaka 2018, Shirika lilipata faida ya bilioni 3.63, mwaka uliofuatia ambao ni 2019 likapata bilioni 7.79, mwaka 2020 likapata bilioni 33.65 na mkwa unaoishia Juni,2022 wamepata bilioni 73.10 hivyo shrika limeendelea kuongeza faida kila kukicha.

Aidha Bw.Msongole amesema kuwa matarajio yao kufikia mwakani kwa maana hesabu za kukaguliwa kufikia Juni 2022 hesabu hiyo itakuwa mbali na hiyo ambayo wamefikia kwa sasa.

Pamoja na hayo amesema kwa mafanikio hayo waliyoyapata wanatarajia kutoa gawio kwa Serikali kutokana na mafanikio makubwa ambayo yamepatikana kwa miaka minne kwa kuongeza mtaji.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina Bw.Mgonya Benedicto amesema Shirika hilo limejiweka vizuri katika kudhibiti matumizi yasiyo na tija na kwa wakati huohuo limeendelea kujenga imani kwa watanzania ambapo hivi sasa ni idadi kubwa kwa wanaokata bima kwenye shirika hilo.

Ameeleza kuwa katika majadiliano yao kupitia mahesabu ya shirika, ile faida ambayo imepatikana sehemu wameamua kuimarisha mtaji wa shirika ambapo sasa utaiwezesha kufanya bioiashara kisheria ukilinganisha na hapo awali vilevile wamekubaliana shemu nyingine ipelekwe kwenye mfuko wa serikali kama gawio kwa serikali.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elirehema Doriye amesema moja wapo ya mipango ambayo wamekuwa nayo kwasasa ni kattika uharaka wa utoaji huduma za Bima, kwasasa NIC linatoa huduma za Bima kwa maana ya ulipaji wa madai kwa muda mfupi kuliko shirika au kampuni yoyote Tanzania, ndani ya siku tano za kazi unapata malipo yako.

CREDIT: Fullshangwe Blog.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here