Home LOCAL NAIBU MEYA SAADY KHIMJI AGAWA FUTARI KWA WAJANE

NAIBU MEYA SAADY KHIMJI AGAWA FUTARI KWA WAJANE

Kheri Shaaban: Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji Saady Khimji akikabidhi Futari kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa Amana Ramadhani Poley Leo April 29/2022 Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Ilala Futari aliyepokea Mwenyekiti Ramadhani NAIBU MEYA SAADY KHIMJI ametoa Kwa ajili ya watu wenye Maalum (nyuma ya Naibu) Mwenyekiti wa Serikali za mtaa Ilala Bungoni Ally Mshauri (PICHA NA HERI SHAABAN).

Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji Saady Khimji (Kulia wa kwanza)akigawa futari katika Ukumbi wa Afisa Mtendaji wa kata ya Illala Leo April 29)2022 Kwa ajili ya kuaaidia watu makundi Maalum na Wajane (Picha na Heri Shaaban).

Na: Kheri Shaaban:

NaibuMeya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Saady Khimji amegawa Futari kwa WAJANE na Watu wenye mahitaji Maalum wa Kata ya Ilala

Naibu Meya Khimji aligawa futari hiyo katika Ofisi ya Kata ya Ilala ambapo alikutana na WAJANE pamoja na makundi Maalum.

“Futari hii ambayo nimegawa Leo kwa ajili ya kuwapa Futari ndugu zangu Mwezi huu ni wa kupata Neema na fadhila za Mwenyezi Mungu”alisema Saady

Khimji alisema Futari hiyo aliyotoa kwa wananchi wake amepewa na wadau wake Shule ya FEZA  International School mwakani atajipanga vizuri kwa ajili ya tukio kubwa kwani anajali mchango wa viongozi na makundi yote ambayo anashirikiana nao vizuri Katika kuleta maendeleo pamoja na kujenga Ilala.

Alisema amefarijika sana Katika jambo hilo kwa kushirikiana na KAMATI ya Maendeleo Kata na Wenyeviti wake wote.

Khimji aliwataka Wenyeviti wake wa SERIKALI za mitaa waendelee kushirikiana Katika utendaji wa kazi sambamba na kuleta maendeleo .

Aliwashukuru Wajane na Watu wenye mahitaji Maalum kuitikia wito wa kikao hicho Maalum cha kupokea Futari hiyo

Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Ally Mshauri alimpongeza Diwani Saady Khimji kwa msaada huo kwa dhumuni la kuunganisha Watu wa Kata ya Ilala pamoja

Diwani wa Viti Maalum Wanawake Kata ya Ilala Asha Kipini alimpongeza Diwani Saady khimji kwa kugawa Futari hiyo pamoja na makundi maalum.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here