Home ENTERTAINMENTS MTWARA FASHION SHOW KUSHUSHA NEEMA KWA MAKAUNDI YENYE UHITAJI

MTWARA FASHION SHOW KUSHUSHA NEEMA KWA MAKAUNDI YENYE UHITAJI

NA: MWANDISHI WETU

MWANAMITINDO chipukizi hapa nchin Rahma Haruba ambaye pia ni muandaaji wa tamasha la Mtwara Fashion Show, amesema mapato yatakayo patikana katika shoo hiyo yatagawanywa katika makundi ya wahitaji katika jamii.

Huu ni msimu wa kwanza wa jukwaa la Mtwara Fashion Show ambao utafanyika Mei 15 katika ukumbi wa Millenium mkoani humo.

Akizungumza na ukurasa huu amesema awamepanga kuwa baadhi ya mapato yataenda kusaidia jamii ya Mtwara katika nyanja ya elimu, afya na watoto wanaoishi katika mazingira magum.

“Lengo letu kiasi tutakacho kipata kwenye shoo hii tutagawanya katika nyanja ya shule za msingi, tutasaidia wanafunzi wenye uhitaji wa nguo za shule, kundi la pili tutapeleka hospital za serikali hapa tutajikita kwa wale wagonjwa ambao hawawezi kujihudumia kutokana na kipatao pia tutapeleka wa watoto ambao wanalelewa kwenye kituo maalum wale watoto ambao wamezaliwa na ugonjwa uitwao usunjo,” anasema Rahma Haruba. 

Mpaka sasa wabunifu wanne, watatu kutoka Dar es Salaam, ambao ni  Didistyle, Baraka, Achiba designer  na mtwara mmoja ndio walio jisajili kushiriki kuonyesha kazi zao kiingilio VIP 30000 na Kawaida 20000.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here