Jeshi la polisi Mkoani Tabora linafanya uchunguzi wa kina kubaina mafuvu na masalia ya miili ya binadamu iliyokutwa katika pori la uyogo kata ya Uyogo wilaya urambo mkoni Tabora.
Akithibitisha tukio hilo mbele ya Mwandishi wa habari hizi kamanda wa Polisi mkoani Tabora Richard Abwao amekiri kupatikana kwa mwili wa mtu mmoja huku masalia mengine wakiendelea kuyafanyia uchunguzi.
Alisema kwamba mwili wa mtu mmoja aliyekutwa amekufa eneo hilo na baadhi ya masalia ya miili na mifupa imepelekwa kwa mikemia mkuu kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kuweza kubaini ni binadamu au kitu kingine .
Kamanda Abwao alisema kwamba jeshi hilo linaendelea na msako mkali wa kuwakamata watu waliofanya mauaji hayo na kuacha masalia mengine ya mifupa ikiwemo mafuvu .
“Tunafanyia uchunguzi juu ya masalia hayo na kubaini ninini chanzo cha mauaji hayo yaliyosababisha mtu au watu kutupwa katika pori la Uyogo na kuutupa mwili wa mtu ambaye jina lake halifahamika ni nani na anatokea wapi kwenye maeneo ya Urambo “alisema kamanda Abwao.
Kuliripotiwa kupatikana kwa mafuvu ya watu waliokufa katika pori lililopo kata ya uyogo ambapo wananchi walilalamika upotevu wa ndugu zao na mmoja alibainika kupotea katika kitongoji cha kitega uchumi kata ya urambo na baadae kukutwa masalia ya mwili na nguo ambazo ndugu zake walizitambua na kulazimika kumzika katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa kijiji cha kasela kata ya Uyogo Tomas Petro alisema awali walibaini masalia ya watu waliokufa katika kisima kimoja kilichopo karibu na pori hilo ndipo jeshi la polisi walifika kwa ajili ya hatua za kiusalama.
Diwani wa kata ya Songambele kati ya kata tatu za Muungano na Uyogo wanaomiliki kikundi cha ulinzi shirikisho kinachojumuisha kanda ya Songambele Aliya Kafwenda alisema wameendelea kuimalisha ulinzi na usalama sio kwa kata hiyo peke yake bali ni kata zote tatu na zingine za jirani.
Kwa mujibu wa viongozi wa kata za uyogo na songambele kwasasa hali ya ulinzi na usalama imeimarika na hakuna taarifa zozote za uvunjifu wa amani kwa siku kadhaa sasa.
Mwisho.